Lengo Letu Watanzania si hili!

Lengo Letu Watanzania si hili!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,200
Reaction score
7,568
Wakuu; kuna jambo naona tukiliweka sawa tunaweza kwenda vizuri zaidi mbeleni.

Kimsingi; Lengo letu watanzania kwa ujumla wetu (Kama Taifa) bila kujali ni nani yuko chama gani, kitengo au sekta gani, ni kuhakikisha nchi yetu inapata maendeleo ya haraka katika maeneo ya kiuchumi na kisiasa wakati huo huo tuki hakikisha kwamba nchi yatu ni salama.Naamini kwamba watu wote wanaofikiri watakubaliana nami katika hili.

Ki msingi hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu mwenyewe, na pia hakuna binadamu mkamilifu, ndio maana kunakuwa na mgawanyo wa madaraka na majukumu katika taasisi yoyote kubwa ili kusaidiana, kukosoana na kusahihishana lakini mwisho lengo linakuwa ni moja; "maendeleo ya nchi yetu".

Tanzania kama zilivyo nchi nyengine, tuna idara,vitengo na vyombo mbalimbali ambavyo vinatakiwa vifanye kazi kwa kusaidiana (complement each other) kukosoana (critisizing) na kusahihishana(indicating the way foward).

Kwa upande wa Chama Tawala na serikali yake, Chombo mbadala ni vyama vya upinzani. Kwa sababu hiyo basi, kwa kuwa ili chombo kimoja kiweze kufanya kazi vizuri, ni lazma kipate nguvu mbadala inayozua changamoto chanya na kuibua mijadala, ili kulifikia lengo letu kama taifa; ni lazma pande zote hizi ziwepo na ziwe na nguvu kubwa.Hata hivyo serikali haiwezi kuwa imara kama hakuna upinzani imara; Hivyo anaeimarisha upinzani, maana yeke pia anaimarisha serikali na kusaidia taifa kuelekea katika lengo letu na hivyo anapaswa kuungwa mkono.

LENGO LETU VS KILE TUNACHOKIFANYA KWA SASA!

Kumekuwa na hali ya kukandamiza upinzani kana kwamba ni taasisi ambazo hazikupaswa kuwepo, au uwepo wake unakwamisha katika kuliendea lengo.Ikumbukwe kwamba serikali ndio taasisi kuu inayoweza kutupeleka katika lengo. Hata hivyo serikali hiyo huundwa na watu wenye udhafu kadha wa kadha. Njia pekee ya kuifanya serikali iweze kutupeleka katika lengo, ni kuwa na upinzani imara mno ambao miongoni mwa mambo mengine; huikosoa serikali inapokosea (kam tunavyojua kwa kukosolewa ni hatua ya kuboresha), Kuwatetea wanaokandamizwa (ikiwa serikali inafanya ukandamizaji),kuchangia katika utoaji wa taarifa kwa umma, kufanya tafiti (tena bila kulipwa), kutoa mafunzo kwa viongozi watarajiwa, kutoa mawazo mbadala na kuchochea mijadala (jambo ambalo ni la afya sana kwa maendeleo ya nchi) na mengine mengi; Ni wazi kwamba katika mazingira haya,hatuku paswa kukandamiza vyama vya upinzani hata kidogo ili tuweze kulifikia lengo letu kama taifa.

KWA NINI HALI IKO HIVI LEO HII?

Katika nchi yeyote wanaweza kutokea baadhi ya watu wanaopenda kuishikilia nchi "State Capture".Watu hawa hutumia mbinu za wazi na siri, hila na halali kuhakikisha kuwa wanaishikilia nchi kwa uwazi, au nyuma ya pazia (kwa kuzidhibiti taasisi zote nyeti kutekeleza matakwa yao).Watu hawa wanaweza wakajulikana na wengine wasijulikane.Ukitaka kuwafahamu, miongoni mwa sifa zao;wanachukia sana vyama vya upinzani na wanapenda kuvipiga vita kwa hoja zisizo na ushahidi wala mantiki.Hali hii hujitokeza kwa kuwa ni vyama vya upinzani pekee vinavyoweza kuibua maovu ya watu hawa.

VYOMBO VYA USALAMA Vs LENGO LETU.

Katika masuala ya kijamii, vyombo hivi vimekuwa vikijitahidi kutimiza majukumu yake na hivyo kutusaidia (Kama taifa) kuliendelea lengo letu, lakini linapokuja suala la siasa, wamekuwa wakiingilia na kukandamiza vyama vya upinzani bila au pamoja na kuelewa kwamba kwa kufanya hivyo, kwa upande mwingine wanasababisha utendaji mbovu wa serikali na hivyo kukwamisha kuliendea lengo letu (kama taifa). Kadhalika wanafanya hivyo bila au pamoja na kufahamu kuwa vyama vya upinzani navyo ni sawa na tairi ya nyuma ya gari ambayo ni lazma isukume tairi za mbele kwa hiyo ikitobolewa ikitoa upepo safari haitakuwa sawa, na sisi sote ni mfano wa abiria ndani ya gari hiyo.

Sababu mbili zinaweza kuwa sababu ya hali hizi ; Ya kwanza ni kutumiwa na watu wanaotaka kuishika nchi kwa maslahi binafsi, Pili inaweza kuwa ni kutokana na kutofahamu vizuri athari za kile wanachokifanya.

NINI CHA KUFANYA ILI KUFIKIA LENGO LETU KWA URAHISI?

Ni lazma kila mtu bila kujali Chama, idara au kitengo alipo; basi afahamu kuwa Taifa ni zaidi ya yeye, zaidi ya Taasisi yake, na zaidi ya chama chake.Ni vyema kila mtu popote alipo akaelewa kuwa laiti kila mtu akiamua afanye mambo kwa masilahi yake,au kundi lake pekee, mwishowe kati yetu hakuna atakayepata anachotaka na tutaishia kwenye machafuko. Ni vyema hata wanausalama wetu wawe ni polisi au idara yoyote, wakafahamu kuwa Tanzania ni zaidi ya kitengo chao hivyo lengo letu (kama taifa) ndilo lengo kuu. Ni vyema wasikubali kutumika na wakafikiri mara mbili juu ya hatari za kutumika hata wakafanya mambo yanayotukwamisha kuliendea lengo letu (kama taifa), kwa lengo la kuridhisha kundi, au mtu fulani. Wafahamu kuwa leo wakikubali kutumiwa na mtu "A" itabidi kesho wakubali kutumiwa na mtu "B" Na hatimae watajikuta wakipoteza utu wao. Msingi wetu sote lazma utusukume kuendea dhamira yetu na yeyote mwenye cheo chochote ajue ana dhamana kubwa kwa wenzake.


 
Kwa kuwa kwa kiwango kikubwa kwa sasa wanaotukwamisha ni baadhi ya viongozi wa ccm, na kwa kuwa humo humo ndani ya ccm bado kuna watu wachache wanaojitambua na wanaofahamu ni nini kinachopaswa kufanyika na nini hakipaswi kufanyika, basi nawajaribu kuwashawishi wale wanaotuharibia, kama hawashawishikiki kwa sababu za kimfumo na waungane na upande unatoa muelekeo sahihi bila kuogopa.
 
Yalee yaleeeee
yapi sasa? mbona hujaweka wazi unachotaka kusema?
behindsofa.gif
 
Inabidi ifike wakati siasa tuziwekee mipaka ili chi iweze kuendelea, maendeleo ya nchi si siasa pekee kuna ukuaji uchumi, jamii, teknolonojia na uthamini wa mazigira. kutambua hili weledi wa vuiongozi wa siasa utaimalika na kuchezea nchi kwa kanda za vyama kutatoweka, ni wakati sasa kuwa na same coarse for national development iwe kwa chama tawala au chama pinzani.
 
Hakuna haja ya maneno mingi. Lengo kuu litabakia kuwa ni kuwang'oa wezi madarakani, nchi haiwezi kuendelea chini ya genge la walanguzi
 
Back
Top Bottom