LEMA: Ni mwendawazimu tu atakataa Rasilimali za Tanzania zisilindwe

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,942
19,130
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amefunguka kuwa hakuna mtu anayepinga ulindwaji wa rasilimali za nchi hii na kudai labda mwendawazimu ndiye anayeweza kupinga, na kuongeza kuwa shida ipo kwenye namna ya ulindaji wa rasilimali hizo.
Lema alisema hayo jana bungeni kwamba nchi saizi imeingia kwenye mgogoro na mgodi wa ACACIA na kudai, mgogoro huo unakwenda kuvunja imani na moyo wa wawekezaji wengi kuja kuwekeza katika nchi hii jambo ambalo linaweza kuipelekea nchi ya Tanzania mbele ya safari kuwa kama Zimbabwe.

"Hatua ya kulinda rasilimali za nchi hii ni mtu mwendawazimu anayeweza asipongeze, lakini namna gani unalinda rasilimali za nchi hii inaweza ikaigharimu taifa hili na kuliingiza kwenye matokeo mengi, Mh Mwenyekiti leo taifa hili wote tunafahamu kwamba nchi hii ina mgogoro na ACACIA Mining, mgogoro huo unajenga hisia na sifa za kisiasa ndani ya nchi lakini sura ya pili ya mgogoro huu unakwenda kabisa kuvunja imani na moyo wa wawekezaji kuja kuwekeza ndani ya nchi hii" - alisema Lema

Mbunge huyo aliendelea kusisitiza
"Mwenyekiti siyo tu ACACIA ukiangalia ardhi kwenye wizara ya Lukuvi imekuwa ni sifa kunyang'anya watu ardhi, imekuwa ni sifa kunyang'anya wawekezaji ardhi jambo hili mbele ya safari litaifanya taifa hili liende likawe kama Zimbabwe, siasa na biashara ni vitu vinavyofanana na mwanasiasa makini ni yule atakayejua maana ya uchumi, hawa wananchi leo wanaoshangilia baada ya miezi miwili mitatu watakosa chakula, wakikosa chakula itakuwa raisi kuingia barabarani" -Godbless Lema

 
mjinga tu kwani wawekezaji wakiridhika na hali ndio wananchi wanaridhika na hali. wawekezaji sio wajomba zetu wanakuja kutafuta faida tu. sisi ndio tuna wajibu kuhakikisha uwekezaji unatuletea maemdeleo sio umaskini. kuliko umma kuletewa umaskini kwa faida ya vigogo fisadi bora wawekezaji jambazi wa uchumi wetu waondoke.
Bila kuwa na sheria nzuri ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
Bila kuwa na sheria nzuri ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
sheria kwa issue hii sio tatizo ila ni hila ya mwekezaji na vigogo serikalini kufanya udanganyifu kuhusu kiwango cha madini wanayopata.
 
Malizia basi yote,
Amesema Kulinda sawa, ila namna gani unalinda ndio tatizo
Huko mbele alikoacha ndiko kwenye mambo ya msingi kabisa kuliko hiyo sentensi moja aliyoinukuu mwanzoni. Kama propaganda hajui kama alitaka kutuamisha hicho anschofikiri yeye alitakiwa akate hiyo clip iishie hapo kwenye sentensi iliyomfurahisha yeye. Sasa ameacha mpaka tumejua kumbe msemaji hayupo na mtoa mada!
 
mjinga tu kwani wawekezaji wakiridhika na hali ndio wananchi wanaridhika na hali. wawekezaji sio wajomba zetu wanakuja kutafuta faida tu. sisi ndio tuna wajibu kuhakikisha uwekezaji unatuletea maemdeleo sio umaskini. kuliko umma kuletewa umaskini kwa faida ya vigogo fisadi bora wawekezaji jambazi wa uchumi wetu waondoke.
Mbona ujauliza walio wapa
 
Nilichoona katika nusu clip hiyo ni Mh. Lema lengo KUU lake ni kulalama kwanin Upinzani usiachiwe ufanye siasa muda wowote.


Serikali ifanyie kazi malalamiko hayo.
 
Back
Top Bottom