Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,432
- 73,078
Mhe.Lema Mbunge wa Arusha ni mwanasiasa mahiri lakini wa viwango vya kawaida kwani wa aina yake bado wapo wengi tuu. Lakini ghafla ametokea kuwa maarufu mno na kuonekana shujaa mbele ya wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla. Hali iliyojitokeza Mjini Arusha leo ni uthibitisho kuwa hakuna wa kumzidi umaarufu wa kisiasa kwa sasa hapo Arusha.
Nini kimesababisha? Ukweli ni kuwa uonevu na wivu wa viongozi wa serikali ya CCM ndio karata yake iliyo mfanya aibuke shujaa wa aina yake. Viongozi hao akiwamo Mrisho Gambo RC wa Arusha wameonyesha wazi kuhusika na njama ambazo Majaji wa Mahakama ya Rufaa wameita 'unajisi wa sheria' dhidi ya Lema.
Safari ya kisiasa inajambo muhimu moja kuu nalo ni kupata uungwaji mkono, na hilo Lema amelimaliza sasa ni shujaa na anaungwa mkono hivyo watesi wake badala ya kumpunguzia umaarufu sasa ndio wamempa kiki zaidi kwa wao kushindwa kujua walilofanya ni kosa kubwa kimkakati kama walivyo dhani mwanzo