Lema na CHADEMA wajipange sawasawa

Lema na CHADEMA wajipange sawasawa

Samaki Singa

Senior Member
Joined
Nov 20, 2016
Posts
191
Reaction score
195
Ni wazi kwamba kujiondoa kwa Meya wa Jiji la Arusha, Bw. Kalist Laizer na kujiunga na CCM kuna malengo maalum ya kuizika CHADEMA katika Jiji hilo.

Laizer ameandaliwa na anajipanga kuwa Mbunge mpya wa jimbo hilo mwaka 2020 kupitia chama kubwa CCM. Mwanasiasa sio mwenzio. Chukua tahadhari!

Capture%2B_2019-11-22-03-49-26-2.jpeg
 
Ni Wapuuzi tu wanaoweza kuwa na mawazo mgando kama huyo, Chadema imeshapitia magumu zaidi ya hayo, kuondoka kwa huyo Kenge wala hakupunguzi kitu aliondoka Zitto na hatukuyumba hususani huyo mburula??
 
CCM wategemee upinzani mkubwa, wajipange kwelikweli maana Lema ni mbishi na wanaArusha wana misimamo
 
Subiri kuyakoga mleta habari, jitahidi leo usikae mbali na glas ya maji babu alisema maji hupoza hasira
 
Kwa sasa naweza kushangaa pale ninapoona kuna mtu bado anajivunia siasa za upinzani kwa mkoa wa Arusha, nahisi huyo atakuwa hajapitia mitaani na kupata picha ya kisiasa.

Kiukweli Lema hana chake Arusha hata mnaotukana kwa tukio la Kalist bado hamuelewi mchezo wa siasa, nini kinawashinda wapinzani kuwatoa watu ccm waje kwenu?
 
Nionavyo hapa TZ kuhusu siasa za vyama vingi ni sawa na mtu akuambie ubuni kanuni ya kubadili maji chumvi baharini kuwa maji baridi.

Abishae na aseme hapa ni kwa jinsi gani chama kilicho shika usukani hivi sasa kitapokonywa usukani.

Waliotengeneza mfumo huu na namna ya kudhibiti bahari isiwe maji baridi wana sababu na nyingi ni nzuri tu kulingana na nyakati.

Vyama vya upinzani huenda vinajua ukweli huu, huenda vinaendelea kufurukuta kwasababu za ubahatishaji. Kwamba, yanaweza tokea makosa ya kiufundi chumvi ikawa sukari.

Ndio maana kuna matukio ya watu kutoka upinzani na sijui ni kwenda au kurudi walikotoka na baadhi ya vyama kuonekana ni vyama pandikizi.

Ni maoni ya raia wa kawaida tu, msijishughulishe sana kufuatiliana au kushambuliana.
 
Back
Top Bottom