Lema adai kuwa, kwa sasa CHADEMA haina Kiongozi anayekaa mbele kuwaonyesha watu waende wapi kama enzi za Ndesamburo

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Katibu Mkuu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema akizungumza na Mwananchi amedai kuwa Madiwani na Viongozi wengine wa Chama cha CHADEMA katika Mkoa wa Kilimanjaro, Mikoa mingine na Taifa kwa ujumla, wanamkosa mtu wa kuwasuluhisha tangu kifo cha Philemoni Ndesamburo mwaka jana 2017.
Lema alidai kuwa, enzi za uhai wa Ndesamburo, alikuwa mtu wa tofauti katika siasa na kiuchumi na kwamba kumkosa tu kwa mwaka mmoja, wamevikosa vitu vinne (04) wanavyovililia kwa Sasa. Moja ya vitu hivyo ni kukosa kiongozi anayekaa mbele kuwaonyesha watu waende wapi kama alivyokuwa akifanya Ndesamburo.

IMG_5694.JPG

IMG_5692.JPG
 
Hii hatari sana. Kulipaswa kuwa na mifumo ya ndani ya chama ya kuwapata wasuluhishi na wapatanishi. Msitegemee MTU.

"Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu"....BIBLE.

Yanayowakuta Yanga pia ni kwasabb walimtegemea Manji.
 
Sio kila mgogoro, sintofahamu au mkwaruzano lazima uzae EXIT. Jamaa ana hoja, ni lazima uwepo utaratibu wa kuwaunganisha wanachama hasa kwenye nyakati ngumu za kutokua na maelewano. Kwenye jamii ya watu wengi ni lazima tofauti zitokee hata makanisani, misikitini, kwenye familia n.k
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema akizungumza na Mwananchi amedai kuwa Madiwani na Viongozi wengine wa Chama cha CHADEMA katika Mkoa wa Kilimanjaro, Mikoa mingine na Taifa kwa ujumla, wanamkosa mtu wa kuwasuluhisha tangu kifo cha Philemoni Ndesamburo mwaka jana 2017.
Lema alidai kuwa, enzi za uhai wa Ndesamburo, alikuwa mtu wa tofauti katika siasa na kiuchumi na kwamba kumkosa tu kwa mwaka mmoja, wamevikosa vitu vinne (04) wanavyovililia kwa Sasa. Moja ya vitu hivyo ni kukosa kiongozi anayekaa mbele kuwaonyesha watu waende wapi kama alivyokuwa akifanya Ndesamburo.

View attachment 824193
View attachment 824192
SACCOS ya wachaga inapata taabu sana hivi sasa na yajayo
 
Laana ya kunyima huyo mzee fursa ya kuwa mwenyekiti wa kanda ya kaskazini na kumpa Jaffari,itawaandama chadema
 
Back
Top Bottom