kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,931
- 7,828
Siasa anazofanya Lema, Mbunge wa Arusha kwa hakika ni za kijambazi. Katika clip ya video aliyorekodi punde utaona si anamtishia amani DPP tu bali viongozi wote wa awamu ya tano.
Wenye ufahamu wanajua aina ya uongozi wa nchi wanayopigania CHADEMA ni ile ya mwenye nacho anaongezewa na asiyenacho anazidi kuwa maskini. Tafsiri halisi ya demokrasia wanayopigania ni pale kuna ulaghai wa uhuru huku wenyenacho wananunua haki na kuuziwa haki kutokana na mfumo wa rushwa na ubinafsi kutawala.
Huko nyuma wahujumu uchumi na fisadi kumekuwa na kesi tu. Kila mwananchi anajua hujuma na ufisadi lakini hakuna anayekamatwa na akikamatwa anashinda kesi hafungwi maana haki inauzwa na wanasheria na wenye nacho wananunua haki.
Ndio maana baada ya tumbuatumbua ya majipu ya kifisadi fisadi wamejaa gerezani. Ni kweli kama anavyodai lema washutumiwa wa ufisadi na ndugu na marafiki zao wana hasira na kisasi. Ila si kama anavyotumaini Lema eti 'regime' hii itapita fisadi watarudi ulingoni na kulipa kisasi.
Kina Lema wajue Watanzania walifunzwa na Baba wa Taifa kudai haki na kupinga unyonyaji ndio maana Mwalimu Nyerere akaita chama alichokiongoza mwenyewe Chama cha Mapinduzi. CCM sio chama cha kiliberali kama CHADEMA kwa sababu kinapigania demokrasia na kupinga unyonyaji wa tabaka moja kulinyonya tabaka lingine.
Ningemshauri Lema atafakari badala ya kuwatisha watendaji na viongozi wa awamu ya tano kupitia kitisho kwa DPP. Ajue hakuna kurudi nyuma, mapinduzi ya uchumi Tanzania yataenda kwa kasi na kumfadisha kila raia.