charz91
Member
- Aug 10, 2013
- 34
- 12
LAZIMA UTOKE JASHO, KISHA UPATE
LAZIMA tuelewe yakuwa mafanikio hayaji kwakuyadhania, yaani madhari tu unafikiria kwamba siku moja utakuwa na maisha mazuri kwa kiwango hicho cha kijidhania kwako na ikawa hivyo, hapana. ni lazima ujishughurishe, mara nyingi watu ujidhania kwamba ugumu wa maisha waliyonayo ni kwasababu ati haijawafika siku ambayo Mungu amewapangiwa waweze kufanikiwa, hizi ni nadharia tu, ambazo hazina nafasi katika ulimwengu wasasa ambao watu wanatakiwa kuacha uvivu wa aina zote yaani wakufikiri na wakutokujibiidisha, hakika kufanya madhanio hayo pasi nakuonyesha juhudi za mapambano ya utafutaji na mbidiisho, kwakweli huo unakuwa ni upuuzi wa hali ya juu.
Tulipokuwa angali wadogo wengi wetu ambao kwa kiasi fulani hatukuwa naugumu katika kupata mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi, tuliamini kuwa maisha yataendelea kuwa hivyo ama kuboreka zaidi kadri tunavyozidi kukua. ni kweli tuliamini hivyo na ndivyo ambavyo wazazi wetu walituaminisha, lakini wakitusisitiza kuzingatia masomo, nidhamu na utii.
Wakati huo binafsi nikiwa mtoto niliamini pia kuwa siku nitapokuwa na nikafika umri kama aliokuwa nao baba yangu kwa wakati huo, basi namimi nitaweza kuwa na maisha kama aliyokuwa nayo baba yangu kwa wakati huo, na nikiamini kuwa nitapata watoto kama baba yangu alivyonipata mimi na ndugu zangu na nitaweza kuwahudumia kama baba atuhudumiavyo.
Sasa huo ulikuwa wakati nikivaa bukta dark blue na shati nyeupe ya mikono mifupi nikibeba begi kubwa lililojaa daftari za kutosha, peremende na biskuti, ni wakati huo ambapo hakuna nilichokuwa nikiwaza zaidi ya kula wali na kuu wa kizungu nikapewa na soda niliyoipenda aina ya Fanta kisha nikalazimishwa kulala mapema ili kesho nisichelewe kuamka na kwenda shuleni.
Unaweza kusema niwakati huo ambao nilikuwa nikiwaza kuwa nitakapokuwa mkubwa nakupata pesa nitanunua peremende nyingi mabox kwa mabox na nitampatia rafiki yangu Amedeus Maduhu mabox kazaa natukawa tunajirambia kila kikicha zisiishe.
Hayo yalikuwa mawazo ya utoto, ndio...... zilikuwa ni akili za utoto, na kama ijulikanavyo kuwa mtoto uwaza mambo yakitoto tu, na inapotokea mtoto akawaza mambo ya msingi hata watu wazima wakayakubali basi hapo utosha kusema kuwa mtoto huyo amekuwa, lakini kama mtoto akawaza mawazo machanga kama vile kufikiri kuwa atakapokuwa mkubwa atajinunulia peremende na kujaza chumba ili azirambe pasi nakuangaishwa na mwingine, hapo wakubwa usema ule msemo usemao "Ni utoto tu akikua ataacha" na kisha kupuuza.
huo ni utoto wenye mambo hayo yakitoto ambayo hata wazazi wetu waliyapitia, na unajulikana vyema na kila mtu mzima, na hili limejithibitisha kwa kila mtu na binafsi nathibitisha sasa kwa kusema kwamba wala siwazi tena kununua peremende na wala sipendi tena Fanta Orange na badala yake sasa napenda zaidi "Castle lager" Naam ni utoto ulikuwa na sasa nimekuwa nimeacha.
Kwahiyo ni kawaida kwa watoto kufanya na kuwaza mambo yakitoto lakini ni aibu kwa mtu mzima.
NILILAZIMIKA kuyasema hayo niliyoyasema hapo juu kabla yakueleza sasa msingi wa makala yangu, Naam.... msingi wa makala yangu nikuwakumbusha wale wengine ambao wameshakuwa lakini bado wanawaza kununua peremende na kujaza chumba ama kuwaza kuwa na watoto, nyumba na magari bila kujua hayo magari na nyumba vinapatikanaje?
Hapa ninawazungumzia wale ambao hadi hivi leo wanafalsafa zile zakusema kuwa Muda wao bado wakufanikiwa, wakijibaraguza "Ati Mungu bado hajapanga siku yangu ya kufanikiwa, kwa maana siku hiyo ( Mungu aliyopanga) ikifika, basi nitakuwa tu na pesa, magari na nyumba nzuri" haya ni maneno ya mtu mzima ambaye jamii tayari imeona ameshakuwa kwa kigezo cha muonekano tu, lakini anapotamka maneno hayo, ndipo wanashindwa kutomtofautisha na yule mtoto anayewaza peremende na biskuti katika utu uzima.
Mtu huyo anayezungumza hivyo yupo nyumbani kwa baba na mama na umri ameshafikisha miaka zaidi ya Ishirini na pengine amefanikiwa kusoma soma kidogo, huyu hataki kujiongeza, hataki kutafuta shughuri yoyote, yeye kila kukicha anashinda sebuni akipokonyana rimoti ya Tv na wadogo zake nyumbani, ugomvi mkubwa waking'ang'aniana kutazama vipindi mbali mbali vya Runinga ama siku hizi wanapenda kutazama movies za series za watu wa Magharibi. Hiyo ni aina moja ya vijana waliookwishatoka kwenye utoto lakini bado wana act yakuwa wao ni watoto, aina nyengine ni hii,
Ni vijana ambao wao toka washindwe kupata nafasi za kuendelea masomo ya kidato cha kwanza ama kidato cha sita ama pengine chuo kikuu, wao waliamua kukaa nyumbani kwa baba na mama wakikodoa kodoa macho na kurandaranda hapa na pale pasi nakutaka kufanya shughuri yoyote ile, hata shuhguri za nyumbani tu, nazo ni shida yaani kusaidia kupika kuchota maji au hata kwenda shambani kwa wenzetu wa vijijini, vijana hawa hukaa tu nyumbani bila kujishughurisha na mara zote ulalama tu kwa wazazi wao wakitaka pesa za matumizi na vocha bila hata kujua namna gani? pesa hizo zinapatikana.
Vijana wengi wa namna hii ndio ambao hushinda mitandaoni kuanzia asubuhi hadi jioni wakipost picha na upuuzi upuuzi, na hiyo imekuwa kama "fasheni" sasa utakuta jumatatu asubuhi saa nne kijana wa miaka 25 anayeishi nyumbani kwa baba na mama yake, anashinda sebuleni aki-post picha instagram na kwachini anaandika "at home with ma young sister" sasa tazama maajabu hayo Wakati muda huo wenzake wa umri wake wakiwa maofisini ama wapo ilala boma, wakijumua mitumba kwenda kuuza, ama sokoni kariakoo wakijumua ndizi na matango kwaajili ya kagenge kadogo walichojianzishia kutafuta pesa mbili tatu, lenyewe liko kwenye masofa ya baba na mama likichezea smartphone aliyonunuliwa na baba baada yakususa kula siku mbili, confident linachati na wadada waki-Nigeria waliopo facebook wakiraghai vijana wapumbavu mithili yake , ili kujipatia pesa kwakua kwao { Nigeria} unemployment problem is at maximum.
Huko ndiko ninakosema kujitoa akili, yaani mtu mzima kujifanya kama mtoto mdogo, kuishi ndoto za Habunuasi, Ama kweli huu ni ujuhana ni ujuha wa hali ya juu, na ni ujuha kwasababu unafanya ushenzi huo ukiwa na ufahamu kabisa kwamba unajididimiza lakini unaendelea kuishi tu kipuuzi namna hiyo
Kama nilivyosema kuwa VIJANA wengi wanakaa tu nyumbani na ati wakiwa na ndoto zile za kitoto ati yakwamba akifika umri fulani atapata anachoitaji pasi nakujua style za utafutaji wake, anasahau, Mungu alisema kwamba "Jisaidie nami nitakusaidia", hii itoshe basi kuwaaminisha kuwa lazima wajishughurishe ili waweze kufikia malengo, kwa maana kuwa Mungu uanza na wale wanaojishughurisha,
LAZIMA WATU WAZIMA WAISHI KAMA WATU WAZIMA, NA WATOTO WABAKI NA UTOTO WAO, KWAMAANA WAKIKUA WATAACHA