Lazima tuisaidie ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lazima tuisaidie ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Jul 2, 2011.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  [h=6]LAZIMA TUISAIDIE CCM SASA.

  Kwa muda mrefu napata shida kujua wapi kama taifa tunaelekea wapi?Maswali ni mengi zaidi kuliko majibu.Kwanza wenzangu tukubaliane kuwa hii ni nchi yetu sote bila kujali dini,kabila,raangi n.k.Katika Tanzania yetu hatuwezi kujadili maendeleo yetu bila kuitaja CCM.Mazuri naa mabaya yote katika kuendeleza taifa hili,CCM haiwezi kukwepa.

  TANU hadi CCM ya chama kimoja,mpaka vyama vingi,ndio hii ya leo.Niseme tu wazi kuwa CCM hapa ilipofikaa ni kileleni,hapa ndio mwisho.Wengi wanapenda sana tuendeleze maashairi ya kuisifia CCM.Wanachama wa leo wa CCM hawapendi sana kukosolewa na kuona wao ndio wana haki na kila kitu katika nchi hii.Katika vitu ambavyo CCM imefanikiwa sana ni kuwafukarisha watanzania na kuwafanya wawe wajinga ili wasijue haki zao.CCM leo ipo madarakani si kwa sababu inapendwa bali ni kwa sababu ya ujinga wetu na mifumo tuliyonayo.Vijana wengi hatuna ajira,hivyo ili uweze kupata ajira basi ni bora ujikombe kwa CCM na kujifanya hamnazo.

  Haya ndiyo yanayotokea mitandaoni.Ni sawa maana kila mtu ana haki ya kuchagua anachopenda,lakini lazima tuzingatie ukweli.Kwa sababu ya utindio wa ubongo,ulevi wa madaraka,kuvimbiwa na kuona wao ndio wana haki ya kuongoza nchi hii,CCM leo inafanya inavyotaka bila kuzingatia hali halisi ya maisha ya watanzania.Madaraka yanawafanya viongozi wetu kuwa vipofu.CCM ina faida nyingi sana ili kiweze kubadilika.Kwanza ni changamoto cha vyama vingi.Lakini kwa bahati mbaya suala la madaraka limekuwa la kufa na kupona.

  Vyama vingi imekuwa ni uadui.Kama CCM wangekuwa na viongozi wanaoona mbali wangetumia fursa ya kuibuka kwa CHADEMA kujiimarisha.Kwa kujua au kutojua CCM inaipaisha sana CHADEMA.Kama CCM wangekuwa wanachukua mazuri yanayosemwa na CHADEMA,leo hii CHADEMA wangekosa agenda.Lakini kwa kuzingatia ukweli,kwa kustruggle na CHADEMA,CCM inachimbia kaburi.

  Mambo mengi yanayozungumzwa na CHADEMA ndiyo yaliyoko kwenye midomo ya wananchi wa kawaida.Kuwapuuza sana CHADEMA ni kuwapuuza wananchi.Sasa kuna dhana ya kujivua gamba.Kubadilika kwa CCM ni kitu kizuri lakini kwa bahati mbaya sana michezo ya kuigiza imetawala katika falsafa hii,ambayo inaoongozwa na Nape.Nawambieni mwisho wa Nape na wengine upo karibu sana.Rais Kikwete ni ndumila kuwili,si mtu ambaye anayeaminika sana.Wakati akitangaza falsafa ya kujivua gamba,rais Kikwete amekutana na wanaodaiwa kukichafua Chama ili kukubaliana jinsi ya kumaliza suala hilo.

  Yapo mengi ya kuandika,lakini niseme tu kama ambayo ukoloni ulijimaliza wenyewe,ndivyo ambavyo CCM inajimaliza kwa kuwa na wanachama wanafiki ambayo hawaamini katika itikadi ya Chama kama akina Samwel Sitta.CCM hapa ilipofika kamwe haiwezi kubadilika.Kuna nafasi nyingi sana ambazo walitakiwa kuzitumia kubadilika lakini haikuwa hivyo.Wananchi tuna jukumu la kuisaidia CCM ili ikae benchi ijifunze.Tunajukumu la kuwaambia ukweli japo tutabezwa na wana CCM masilahi waliojaa kila kona.Tafadhali sana wananchi tuisaidie kuiangusha CCM kama kweli tunataka maendeleo.Narudia tena kwamba CCM kamwe haiwezi kubadilika,kama wengi mnasubiria mabadiliko katika CCM poleni sana.Nipo tayari kwa challenge.
  [/h]
   
Loading...