Lazima kutoa sadaka Kanisani

Job Richard

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
3,876
2,187
Makanisa mengi imeonekana kumekuwa na ulazima katika kutoa sadaka PASIPO KUANGALIA MIOYO YA WAUMINI NI kawaida mchungaji analichika kapu la sadaka na kusema mbona kidogo watu hawamtolei Mungu atawasema sana
WENGINE WAMEVUKA ZAIDI WANAWAPANGA WATU KWENYE MAKUNDI KUTOKANA NA ANACHOTOA

kuanzia elfu kumi mbele chini ya hapo nyuma ni haki hiyo

MATHAYO 5;23 ukileta sadaka yako ukikumbuka ndugu yako ana neno juu yako (umemkosea) RUDI UKAMWOMBE MSAMAHA NDIPO UTOE SADAKA YAKO

Lakini sasa hivi hatuangalii haya
 
Pia utoapo sadaka iwe ni kwa siri, hata mkono wa pili usijue, lakini nashangaa kwenye makanisa ya sasa wanajazishwa form za sadaka, na wale watoao zaidi wanapewa heshima tofauti na wale watoao kidogo
 
Na mwanaume ukigombana na mkeo, maombi yako hayasikilizwi hadi utakapoweka mambo sawa.......
 
Pia utoapo sadaka iwe ni kwa siri, hata mkono wa pili usijue, lakini nashangaa kwenye makanisa ya sasa wanajazishwa form za sadaka, na wale watoao zaidi wanapewa heshima tofauti na wale watoao kidogo

hili jipu wanakuangalia umekuja na nini V8 UNAHESHIMIWA wale kajamba nani kwa miguu hata hawashughuliki nawe DINI ZA PESA KWANZA UTU BAADAE SIKU HIZI
 
Kweli mambo ya kuandika sadaka kwenye fomu,hayana tija kabisa.Wengine tukiona hivyo lazima tusepe.Halafu inakuwa lazima utoe sadaka makapu hata 6 yote michango bado Jumuiya sijui zilete marejesho.Bora nijianzishie kakanisa ka nyumbani mwenyewe
 
hahahah sema ni kumuomba Mungu tu maana haya makanisa wamefanya mitaji
 
Mkiwa hamna sadaka muache kwenda kanisani

Kwa hiyo unaona ni sahihi kutoa sadaka katika mfumo huu SADAKA LAZIMA IFUATE NENO LINASEMAJE unatoa sadaka huku nyumbani no maelewano sio sadaka
 
Pia utoapo sadaka iwe ni kwa siri, hata mkono wa pili usijue, lakini nashangaa kwenye makanisa ya sasa wanajazishwa form za sadaka, na wale watoao zaidi wanapewa heshima tofauti na wale watoao kidogo
Aliye nacho ataongezewa na asiye nacho hata kile kidogo alichonacho atanyang'anywa....Umeshaambiwa hapo juu usiende kanisani kama huna michango...ila ile ya kanisani sio sadaka ni michango....kama ilivyo michango ya harusi.
 
Bila sadaka mchungaji na familia yake watakula nini? Watavaa nini? Wataishi wapi? Maana hiyo ndio ajira yake na kila ajira inastahili ujira; Na ujira wa mchungaji ni kupitia sadaka zenu.

"Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu;" - Luka 10:7-8

"Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi? Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili." - 1 Wakorintho 9:7, 11, 13, 14
 
Kweli mambo ya kuandika sadaka kwenye fomu,hayana tija kabisa.Wengine tukiona hivyo lazima tusepe.Halafu inakuwa lazima utoe sadaka makapu hata 6 yote michango bado Jumuiya sijui zilete marejesho.Bora nijianzishie kakanisa ka nyumbani mwenyewe
Io michango na sadaka zisizoeleweka ndio vinakimbiza vijana makanisani na kwenye ibada zingine kama jumhiya
 
Nafikiri ninyi mnaandika na kusema msicho kijua sadaka inafanya mambo mengi katika jamii.watu wengi tena wasiokwenda hata makanisani ndiyo wanao lalamika kuhusu kutoa sadaka kwa sababu hakuna sadaka inayotolewa bira kuwa na maelezo wala kuainisha matumizi yake.
 
Let say unatoa mchango kwa ajili ya kanisa kufungua kituo cha radio au television, obvious lazima waumini mtoe vilivyo vinono kufanikisha hilo. Coz ukipima ni wangapi watafikiwa na neno la mungu kwa njia tu ta radio....yani hakika baraka zake hazina mfano..
Kingine tafuta mtu ambaye ni mwaminifu kwenye utoaji halafu kafilisika...Ukimpata basi sote tutaacha kutoa Sadaka.
Kuna mibaraka mingi sana kupitia utoaji..na ni kupitia utoaji tu ndio Mungu aliruhusu tumjaribu..Hivyo mpendwa tuendelee kujifunza zaidi.
 
Siku hizi kuna matangazo radioni na kwenye tv ( wanalipia) ya wapi kanisa la mchungaji fulani lilipo au matangazo ya barabarani linakuelekeza wapi kanisa lilipo,unadhani wanafanya hivo hili iweje ??????
images
 
Makanisa mengi imeonekana kumekuwa na ulazima katika kutoa sadaka PASIPO KUANGALIA MIOYO YA WAUMINI NI kawaida mchungaji analichika kapu la sadaka na kusema mbona kidogo watu hawamtolei Mungu atawasema sana
WENGINE WAMEVUKA ZAIDI WANAWAPANGA WATU KWENYE MAKUNDI KUTOKANA NA ANACHOTOA

kuanzia elfu kumi mbele chini ya hapo nyuma ni haki hiyo

MATHAYO 5;23 ukileta sadaka yako ukikumbuka ndugu yako ana neno juu yako (umemkosea) RUDI UKAMWOMBE MSAMAHA NDIPO UTOE SADAKA YAKO

Lakini sasa hivi hatuangalii haya
"..Siku hizi za karibuni inaonekana sadaka ni pesa tu, na kwenye makanisa kuna vikapu zaidi ya vi tano kwa ajili ya sadaka. lakini sadaka ya kweli ni kumpa chochote mtu aliyena na uhitaji.."
 
Back
Top Bottom