LAWYERS mpooo?

Maana yake lawyers ni watu wa mapenzi zaidi au nini?
 
Hizi ndio pumba gani sasa uzi hauna kichwa wala miguu wala haiwahusu wanasheria labda wanasiasa!
 
Katika historia ya maisha ya binadamu, amekuwa katika mapambano ya kuutafuta na kujihakikishia uhuru...(mfano
katika simulizi za maandiko matakatifu Adam na Eva/Hawa waliposhawishika kula lile tunda ilikuwa katika jitihada za
kujihakikishia uhuru, nimetoa mfano huu kwani inasadikiwa kuwa Biblia ndicho kitabu kikongwe zaidi katika historia ya binadamu) Hata watu/mataifa yalipopigana vita ilikuwa ni kwa ajili ya uhuru...hata zama hizi mataifa na matabaka ya watu wanapambana kwa silaha au kwa itikadi/mfumo kuwania ama uhuru wa mawazo/kujieleza, uchumi, siasa, Kutobaguliwa, kutembea/kusafiri, kutambuliwa, kuabudu, nakadhalika. Katika mfumo wa kidemokrasia uhuru wa watu huhakikishwa na sheria za nchi na hasa sheria mama(Katiba), ndio maana endapo sheria yeyote itakayotungwa na bunge ambayo itaenda kuubana/kuuondoa uhuru wa wananchi basi Mahakama itakuwa sahihi kuipiga marufuku sheria hiyo kwa sababu siyo ya haki....Hayo ndiyo mahusiano ya uhuru na sheria
 
ndugu yangu vitu kama huvijui kaa pembeni mwanasheria yeyote aliye iva anaielewa vizuri sana hiyo picha na imebeba ujumbe muhimu sana katika uhuru wa sheria,
mkuu tumekusoma sisi Learned Brothers and sisters
 
Learned wa wapi sasa kuna ujumbe gani hapo kama sio pumba kwa hiyo wanasheria mpooo wafanyeje waangalie sanamu au wakaiweke sebuleni usomi mwingine bhana
 
Learned wa wapi sasa kuna ujumbe gani hapo kama sio pumba kwa hiyo wanasheria mpooo wafanyeje waangalie sanamu au wakaiweke sebuleni usomi mwingine bhana
acha ukilaza wako hiyo ni lugha ya picha greater thinker wameisha pata message iliyobebwa na hiyo picha nenda darasani siyo kubisha tuu vitu hata huvijui.
 
Usingekuwa kilaza usingekuwa unajinasibu kiasi hicho kuhusu elimu yako feki EngLbertm wasomi hawana lugha hizo na hawatoki mapovu ovyo kanitafutie solution ya equations za Albert Einstein kuhusu Relativity nijue kweli umepiga umande au haizuru nimwagie tu Poisson's and Laplace's joint equations
 
Last edited by a moderator:
hiyo ndio unaonyesha ni jinsi gani upeo wako mdogo usitegemee mhandisi atakuwa anaweza kufanya operation ya binadamu ndio maana kama kuta kuwa na mjadala wa mainjinia humu ndani sisi wengine tuta kaa pembeni lakini hatuta jifanya tuna jua nakuanza ku critise.
 
ukiona mtu anajifanya kipanga wa kila kitu ujue huyo mtu ana matatizo kama kitu hukijui kaa pembeni waachie wenye anga zao.
 
Learned wa wapi sasa kuna ujumbe gani hapo kama sio pumba kwa hiyo wanasheria mpooo wafanyeje waangalie sanamu au wakaiweke sebuleni usomi mwingine bhana

Mkuu ujumbe hapo ni kwamba "Uhuru na Haki" lazima viende pamoja.
 
Hii picha haina maana yoyote ya maana,mtu kachora tu malesbian wanayonyana ndimi huku mawevishwa mavazi ya noble profession,its a satanic thing......
 
haina ubaya Mapenzi ndio nguzo ya jamii bila mapenzi ungekuwepo wewe??
 
Uhuru na haki ni usomi wa wanasheria? na kilaza maana yake injinia? kumbe usomi sio uanasheria peke yake! Ndo ujue basi kutokuwa mwanasheria tafsiri yake sio ukilaza manake hata wewe kwa mainjinia ni kilaza. Hapa tuweke mada universal sio kujibaraguza mara ooh wanasheria mpooo umeambiwa hili jamvi ni la wanasheria na kama wanayajua tayari hayo masanamu kiundani umeyaleta hapa ili nini nyie ndo mkipika pilau mnapikia juu ya paa kila mtu ajue mshamba leo kajikomboa. Hayo ni masanamu tu ya Freemasons yanayotangaza dini za watu na vilaza ndo wameshikia bango kuona ni fasihi ya kianasheria.
 

Wanadamu ni wabinafsi sana. Ukiruhusu ndoa ya LIBERTY NA JUSTICE haitokuwa na tofauti sna na tuyaonayo Tanzania....UHURU (wa mwenye uwezo wa uchumi) unafanya hata JUSTICE isiwe na NGUVU.....

UHURU BILA WAJIBU ni VURUGU....Wacha vibakie VIKIWA NA MWIKO WA KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI; waheshimiane. wapendane (kama kaka na dada) na, kamwe wasiTAMANIANE....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…