Lawama kwa trafiki kuwa hawakusanyi fedha za fine za kutosha ni uonevu kwa wananchi na kutofikiri kwa makini

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
11,207
18,999
Juzi hapa katika kusafiri kwangu askari mmoja wa trafiki aliniambia wana shinikizo kali kutoka juu kwamba mapato ya fine wanayokusanya yamepungua hawafikii malengo ya fine za barabarani wanazopangiwa. Aliniambia hii imefanya hata wakikukuta na kosa dogo sana ambalo kawaida ni la kupewa onyo, watalazimisha ulipe fine. Akasema hata wao wanajisikia vibaya kwa kuwa wanajua kwamba wanafanya uonevu!

Aliponiambia hivyo nilijiuliza sana, kwamba hivi nchi hii inakuwaje tuna viongozi ambao wanashindwa kutafakari vitu vidogo kama hivi na kuwashinikiza askari trafiki wakusanye mapato zaidi katika hali ambayo sasa inaelekea kwenye uonevu? Je viongozi wetu wameshindwa kuelewa kwamba kwa sasa lazima kuwe na mapatao kidogo ya fine za barabarani kwa sababu zifuatazo?
  1. madereva wengi sasa wamekuwa makini sana barabarani katika kufuata sheria, hasa spidi kwenye vibao vya 50km/hr, kiasi kwamba trafiki sasa wanakamata watu wachache zaidi barabarani kwa kosa la spidi kuliko huko nyuma
  2. watu wenye magari wamekuwa makini zaidi katika kuhakikisha magari yao yako katika hali ya kufuata sheria za barabarani, kutia ndani kuwa na fire extinguisher, kufunga mikanda na pia kuona gari ina taa zote zinazofanya kazi
  3. watu wengi wameamua kutumia njia mbadala kama ndege na mabasi na kuacha kuendesha magari yao binafsi kwenda safari za mikoani. Kila dereva anakuambia siku hizi kuendesha gari kwenda mikoani unaingia gharama kubwa kuliko kukata tiketi ya ndege, hivyo ni afadhali upande ndege au basi
Na pia, jambo ambalo TRA watakuambia ni kwamba mapato ya serikali katika mafuta ya magari yamepungua, kwa sababu watu wengi wameacha kutumia magari binafsi kwenda mikoani na hata mjini.

Hivyo basi, Mheshimiwa Raisi Magufuli, wakati serikali inakaza uzi trafiki wawalime madereva barabarani hata kwa kuwaonea ili fedha zaidi zikusanywe, mapato yanayotokana na uuzwaji mafuta ya magari yanazidi kupungua - total effect ni zero increase au hata decrease ya revenue!

Talk of shooting yourself in the leg!
 
Kama kuna shinikizo basi linatoka kwa viongozi wa jeshi la polisi, kwa sasa viongozi wa juu wa hili jeshi ni aibu tupu, full kujipendekeza ili waonekane wanafanya kazi hata kama inawaumiza wananchi. Jeshi la polisi ni obsolete na uwepo wake hauna maana, wananchi hali ikiendelea hivi itatubidi tujianzishie system zetu wenyewe za ulinzi kwa sababu watu waliopaswa kufanya hiyo kazi wamegeuka kuwa watesi na wanyang'anyi kwetu.
 
Yaani wamekuwa wakatili sana, makosa madogomadogo lakini wanakomaa sana, acha watafute vyanzo ndio uwezo wao umefikia hapo
 
NURU na GIZA huwa havishindani.
...
NIngekuwa msikivu ningewaunganisha raia wenzangu tupaki magari kwa wiki moja tatizo "kila mtu anakufa na hali yake''
 
Yes kwa sababu vyuma vimekaza usawa huu wa kuchangia serikali 30 hamna tunakuwa makini sana barabarani
 
Back
Top Bottom