Lavalava kashikilia nafasi ya mtu WCB

Lavalava kashikilia nafasi ya mtu WCB

Emmaloy

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2017
Posts
216
Reaction score
231
Kiufupi nianze tu kwa kusema watu wengi sio waumini saaaana wa aina ya muziki anaoufanya msanii Lavalava. Kwa muda mrefu sasa style yake ya uimbaji imekuwa haiendani kabisa na aina ya muziki unaofanywa na wasanii wenzie walio katika record label moja. Katika tamasha kubwa la burudani la Wasafi Festival lililopita mikoa kadhaa kabla ya jana kufikia tamati jijini Dsm huyu jamaa perfomance yake steijini imekuwa ya kiwango cha chini saaaana hakuna cha maana anachofanya zaidi ya kutuambia tu watazamaji kuwa hatusikii kwahiyo tuimbe wote..”Nasema siwasikii tuimbe wote tena..”

Ninachokiamini huyu jamaa ile nafasi yake pale WCB haikupaswa kuwa yake ila ni zali tu limemdondokea akajikuta keshasainiwa, tunahitaji watu wenye uweledi wa hali ya juu katika kufanya muziki na sio kila siku kuwa na aina ileile ya uimbaji na mbaya zaidi ni kwamba sijawahi muona akifanya show yake binafsi mbali na kudandia Festival tofauti na msanii Mbosso Khan ambaye hana muda mrefu saaana tangu asainiwe lakini kazi anayoifanya imeonekana

NB: Lavalava kashikilia nafasi ya mtu WCB
Adjustments.JPG
 

Attachments

  • Adjustments.JPG
    Adjustments.JPG
    156.6 KB · Views: 10
Acheni kumzibia riziki jamani, akitoka hapo unataka akaishi vipi kiongozi?

Sio kumzibia riziki...rai yangu ni jamaa inabid ajitume sana ili azidi kwenda mbali zaidi coz tangu mda mrefu sasa yeye ndo kama anaonekana anazidi kurud nyuma
 
Ni kweli, mleta mada yupo sahihi kabisa,lavalava akitoka nje ya WCB hatoboi.
 
Huyu anaimba nyimbo za chumbani. ili umuelewe inabidi uwe na mood flani hivi au umekumbatia ziggo
 
Kama kuimba ni rahisi kama ulivyoandika ebu anza kuimba na wewe tuone...binaadamu amuendelei kwasababu ya roho mbaya
 
Umemaliza kila kitu mkuu. Nadhani anapaswa kujituma zaidi ili aendane na Kasi ya wenzake maana Amepoa Sana ukilinganisha na wenzake . Mwingine ni kwini dalingi nadhani nayeye pia kakalia nafasi ya mtu pia.. Emmaloy,
 
Nyimbo anazoimba ni za utulivu hawezi kurukaruka ovyo
 
Huyu muimba qaswida tu hamna kitu, Queen dareen nae yule alifaa awe muimba kwaya.

Rayvan ndo asset ya WCB .. mondi ni subject inayojituma nakutumia kipaji + energy zote.
 
Back
Top Bottom