Last week of smear campaign beware

George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2008
Posts
470
Reaction score
149
Ndugu zangu Watanzania wote,

Napenda kuwatahadhalisha tuwe makini na propaganda za kipuuzi ambazo imekuwa ni kawaida sana kwa vyama tawala barani afrika kuwatisha wananchi au kuwachafua wagombea ambao wanaonekana tishio kwa uhai na maslahi ya vyama hivyo.

Sote tunafahamu ifikapo jumapili ya wiki hii watanzania wengi waliojiandikisha watajongea kwenye vituo vya kupiga kura na kufanya maamuzi ambayo yatatoa mustakabali wa taifa na maisha yao kwa miaka 5 ijayo.

Hivyo basi imekuwa kawaida sana kwa chama tawala kuandaa kashfa au matukio ya kutengenezwa ambayo wananchi huaminishwa kuwa ni kweli ili kuwafanya wasichague mgombea husika wa chama mbadala au kuwakatisha tamaa kabisa wananchi wasiweze kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Sote tunakumbukumbu nzuri sana ya uchaguzi wa kwanza toka mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1995 ambapo chama cha wananchi CUF huko zanzibar kilikuwa na nguvu kubwa sana na wachambuzi wa mambo wanasema kilishinda uchaguzi huo na kikaporwa ushindi, hata hivyo wiki ya mwisho ya kampeni aliibuka Inspector General wa polisi wa wakati huo, Ndugu Mahita Omar na kuwatuhumu CUF kuwa wameagiza shehena ya visu,Majambia na mapanga kwa ajili ya kufanya fujo, vurugu na maafa. Lengo la chombo hicho cha dola ilikuwa ni kuwatisha wananchi waigope CUF na wainyime kura, cha kushangaza baada ya uchaguzi kuisha na ccm kupora ushindi wa wazanzibar swala hilo lilipotea na hakuna aliyekamatwa wala kushitakiwa.

Baada ya uchaguzi kupita watu welevu waligundua kuwa huo ulikuwa mkakati mahususi wa ccm kwa kutumia jeshi la polisi na IGP Mahita kuibeba ccm.

Hali kadhalika mwaka huohuo huku bara kulikuwa na nguvu kubwa sana ya mabadiliko chini ya NCCR-MAGEUZI na Agustine Lyatonga Mrema ambapo wananchi wlitishwa sana hasa vijijini kuwa wakichagua vyama vya ushindani kutatokea vita kama ya Rwanda na Burundi na wakati huo Rwanda Genocide ndo ilikuwa bado mabichi kwenye vichwa vya watanzania na wimbi la wakimbizi ndo Lina sumbua mataifa na nchi yetu, hivyo basi watu walitishwa sana na kukumbushwa kuwa kuchaguwa upinzani ni kuitumbukiza nchi kwenye maafa kama ya Rwanda. CCM walikwenda mbali hata baadhi ya sehemu za nchi waliwaonyesha watu video za mauaji ya kimbali ili kuwatisha watu na kuwafanya wasipigie kura wapinzani wao.

Propaganda hizi za siku ya mwisho zimekuwa na ufanisi mkubwa sana kwani hupangwa na wanamkakati wenye ubobezi wa hali ya juu kwenye maswala ya propaganda na saikolojia.

Huko zanzibar wamekuwa wakiwaaminisha wazanzibar hususan wa unguja kuwa wakichaguwa CUF na maalimu SEIF SHARIFF HAMAD sultani atarejea tena na kutawala zanzibar,

Hali kadhalika CCM wamekuwa wakitumia propaganda ya kuwagawa watanzania kwa imani zao za kidini na huu ni mkakati uliotumiwa kwa umahiri mkubwa sana pale ccm walipo msimamisha mgombea wa Kikristo na wanahitaji kura za wakristo hususani walipomsimamisha Mzee Mkapa walijitahidi Kwa umahiri mkubwa kuaminisha umma wa watanzania kuwa chama cha CUF ni chama cha waislamu wenye itikadi kali. Lengo kubwa la ki mkakati la ccm ni kuhamasisha wakristo wengi wakapigie kura ccm kukikomoa chama cha CUF.

Hali kadhalika mwaka 2005 ccm walipomsimamisha Raisi Kikwete walitaka kura nyingi za hila toka kwa waislamu na walidiriki hata kutumia gilba ya mahakama ya kadhi ambayo iliota mbawa hapo baadae.

Kama kumbukumbu yangu ni nzuri mwaka 2010 CCM walijutia uamuzi wao wa kuweka mahakama ya kadhi kwa kuwa ghilibu waislamu ili waweze kupata kura zao na hali walikuwa wanajua hawataweza kutekeleza swala hilo.

Timu ya mkakati na propaganda ya CCM ilijipanga tena 2010 kuwachezesha shere watanzania na kuja na propaganda ya kipuuzi kabisa kuwa chama kilichokuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi CHADEMA kuwa ni chama cha kikatoliki eti kwa kuwa katibu mkuu wake na mgombea uraisi ni mkatoliki.

Hiyo propaganda ya ku label CHADEMA kuwa ni chama cha kikatoliki, ulikuwa ni mkakati wa ccm kupata kura za huruma kutoka kwa waislamu na madhehebu mengine ya kikristo ambayo siyo RC, hiyo propaganda ya ukatoliki haikuishia hapo bali walienda mbali zaidi na kuaminishi uma kuwa chadema ni chama cha kazikazini tu. Kama ilivyokuwa kwa NCCR-MAGEUZI mwaka 1995 kuwa labeled Kama chama cha wachaga.

But uchaguzi huo ulipita na yaliyotokea sote tunayafahamu,

Mwaka 2015 tukiwa tumebakiza siku 5 tu tukapige kura, kwanza CCM hawakusubiri wiki ya mwisho kurusha makombora ya propaganda zao kwa chama cha chadema na umoja wa vyama vya UKAWA, Wamejaribu kila mbinu ya ghilba kwenye vitabu vyao vya siasa chafu lakini nyingi zimeshindwa kufikia malengo jinsi walivyo tegemea,

Kwanza campaign ya CCM ya mwaka huu itaingia kwenye rekodi ya kampeni chafu na za kishenzi (barbarians campaign) zilizo wahi kufanyika toka misingi ya taifa hili iasisiwe, kampeni ya chama cha zamani au kikuukuu ililenga zaidi kushambulia watu binafsi yaani wazungu wanasema character assassination or smear campaign and politics of everything goes, tumesikia mambo mengi ya aibu yakizungumzwa kwenye majukwaa mbele ya mgombea wa ccm mambo ambayo hayawasaidii watanzania lakini lengo kubwa lime kuwa ni lile lile la miaka yote ni kukinusuru chama cha zamani.

Mwaka huu CCM wameweka pembeni agenda yao ya kuwa CHADEMA ni chama cha wakatoliki kwa sababu wamesimamisha mgombea mkatoliki na wanataka kura za wakatoliki, adui wa CCM mwaka huu wa uchaguzi ni walutheri ambao mwaka 2010 walizitaka kura zao na walikuwa marafiki zao dhidi ya wakatoliki CHADEMA!, watanzania tuwe makini kwani watu hawa hawaoni haya wala aibu kuligawa taifa vipande vipande ili washinde uchaguzi, kwani wao ndo wamekuwa mabingwa wa kutumia udini na ukabila kuwagawa watu ili washinde uchaguzi, tukatae hizi propaganda mwaka huu.

Tarehe 25, October 2015 siku ya jumapili sisi sote kwa umoja wetu tukapige kura tuwachinje na tupeleke ujumbe CCM kuwa mwaka huu #HATUDANGANYIKI

Hata hivyo Kama chaguzi zote Wiki hii ya mwisho tumenza kushuhudia propaganda za ajabu kwenye mitandao ya kijamii na majukwaani zilizopikwa kwa ustadi mkubwa wa wataalaamu kama kumpakazia Mh Mbowe na kuuza chama na kuhamisha pesa nje ya nchi, tumeona magazeti ya kimkakati ya CCM kabisa kutetea CCM na serikari yake ili kulinda maslahi yao na sio kuangalia maslahi mapana ya nchi.

Tumeona videa ya Mama Regina Lowassa akidhalilishwa kwenye mitandao ikijaribu kukatisha watu tamaa,
Tumeshuhudia njama za kijasusi za CCM wakidiriki kuiba behind the scene clip za studio ya ITV ikimwonesha Lowassa anakohoa sana, na kutumia Kama turufu Yao ku aminisha umma Edward Lowassa ni mgonjwa na hafai.

Tumeona propaganda ya vijana wanaosadikika eti kupewa mafunzo ya kijeshi msituni eti wakijiandaa kufanya vurugu na vijana hao eti inasemekana ni wa vyama vya upinzani!

Na tutegemee propaganda nyingi za kutisha zaidi. Siku hizi chache zilizobaki lengo lake ni kuwatisha watanzania wasichague vyama vya ushindani hususani UKAWA.

Lakini nilicho shuhudia mwaka huu ni mwaka ambao ni wa tofauti kidogo pamoja na nguvu kubwa ya kupinga mabadiliko lakini nguvu ya kutaka mabadiliko ni kubwa zaidi hivyo hata hawa jamaa zetu wa CCM wakija na propaganda gani ya kutu gawa vipande vipande watanzania ili waendelee kututawala tusimame imara na tumuombe mwenyezi mungu atupe ujasiri wa kubadilisha nchi hii.

Nawatakia siku njema na kuwatia moyo tusonge mbele na mapambano kwani Raisi Obama baada ya kuandamwa na siasa chafu mwaka 2008 alisema na nukuu;

"if you dont have any fresh idea then you use stale tactics to scare the voters, you make big election about small things" mwisho wa ku nukuu .

Tafasiri yake isiyo Rasmi ya nukuu ya Obama,
"ukipungukiwa na Mawazo mapya inakubidi utumie mbinu za kuchelewesha kwa kuwatisha wapiga kura, uchaguzi muhimu na wa kihistoria mnaufanya wa kuongelea vitu vidogovidogo"
 
HOngera sana kaka

Mwaka huu hatudanyiki

Hata Lowasa akijitoa sasa hivi bado CCM hatuipi kura
 
Analysis nzuri mkuu.... Unachukua, unaweka .. Lowassa in Kingunges voice.... baada ya hapo. ..unahesabu miguu 200 unalinda kura mpaka kieleweke.... Mungu yuko nasi tutashinda....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…