wakuu naomba msaada wenu nilikuwa nikifuatilia laptop maana nataka kununua sasa mtu mmoja niliongea akaniambia toshiba ni nzuri,kwa walio na uzoefu wa laptop naomben mawazo yenu
laptop nzuri inategemea na mtumiaj mwenyewe anataka nini kila mtu atakwambia anayotumia yeye ndiyo nzuri. Kwangu mimi sony vaio, mac, na hp probook 4530s ndo nzuri
Ili upate ushauri mzuri tueleze bajeti yako na kazi unazotaka kuzifanya ( au shughuli zako) hapo utapata ushauri sahihi, la sivyo tutakuwa tunabahatisha tu.