barach pwm
Member
- Sep 2, 2012
- 43
- 5
Nikuambie ukweli kutokana na experience ya muda mrefu ya laptops, Brands bora kwa sasa kwa laptops zinazotumia Operating system ya Windows ni hizi hapa katika mfululizo wa kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho ni HP, Toshiba, Dell, Samsung, Lenovo. Hata kwa mauzo mwaka jana 2012, HP waliongoza kwa Kampuni zilizofanya mauzo mengi sana ya laptop na bidhaa nyingine. Watu wanalalamikia HP either itakua alipata mbovu wakati ananunua au sio genuine. Lakini katika kampuni ambazo wanauza Quality laptops ni HP, hata ukiangalia kwenye maduka mengi ya laptops bei za HP laptops ziko juu ukilinganisha na zingine, Toshiba nayo ni hivyo hivyo, Dell wamekuwa wakilalamikiwa hata duniani kuwa ubora umepungua ukilinganisha na ilivyokuwa zamani, na hio pia ikasababisha mauzo yake kushuka sana mwaka jana, HP wana historia ya Ubora kitambo sana na wame-maintain hio standard. HP, Toshiba na Samsung wako vizuri. kuna HP Probook 4530s au HP Probook 4555 ziko zinapatikana kwa bei kama yako unayotaka ya laki saba, inakaa na charge zaidi ya masaa 5 ikiwa inatumika, speed nzuri kabisa na ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi data. Ukitaka laptops nzuri na kama upo Dar es salaam, tembelea duka moja liko Posta ndani ya jengo la JM Mall, linaitwa Freedom Communications. Wana laptops za brands nyingi na bei zao ni nzuri ukilinganisha na maduka mengi sana mjini.
Kwa HP mkuu product ipi naweza pata ambayo ipo recent kwa sh laki tisa.,ukinitajia model na specification zake itakuwa vizuri zaidi