mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,072
LAPF ni moja ya mifuko ya pensheni inayofanya vema kihuduma,kiusimamizi na utoaji wa mafao hapa Tanzania.Lakini pia LAPF ni moja ya mifuko ya hifadhi ilioshiriki katika kupendezesha mwonekano wa jiji la Dar es salaam kupitia uwekezaji katika majengo makubwa ya kibiashara.
Sekta ya uendelezaji majengo {Real estate} imekumbwa na mtikisiko kibiashara kwa miradi mingi iliokamirika kukosa wateja hata kupekelekea mengi ya majengo yaliogharimu fedha nyingi {mabilioni} kuwa wazi kwa asilimia zaidi ya 50,na mengi yatakwenda kuwa wazi zaidi baada ya zoezi la kuhamia Dodoma kukamirika.Mfano,Rita Tower,Uhuru Height,Majengo pacha ya PSPF,LAPF Millenium Towers,NHC house,GEPF house,Waterfront,Mindu street towers,Mawasiliano towers,Various Masaki/Oysterbay apartments...
Napata wakati mgumu kuelewa mantinki ya taasisi kama LAPF kanda ya Dar es salaam kwenda kupanga katika jengo la Diplomatic pale makutano ya Mkwepu/Makunganya/Karuta huku wakiwa na majengo mazuri na yenye nafasi zilizo wazi kilometa chache toka mjini..Taasisi nyingi zinahama katikati ya mji sababu ya kero mbalimbali na kuepusha misongamano iweje taasisi inayosimamia michango ya wafanyakazi isijinyenyekeshe katika matumizi ili kuleta tija na faida kwa walengwa ambao ni wastaafu wa sasa na kesho.
Ipo haja ya SSRA kuwa na meno zaidi katika kufanya upembuzi yakinifu wa miradi inayowekezwa na taasisi hizi {GEPF,LAPF,PPF,NSSF,PSPF,n.k} lakini pia matumizi yenye tija yapewe kipaumbele kwa maslahi bora ya washikadau