Langa tutakukumbuka Daima

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
643
845
Hii mistari imenifanya nimkumbuke sana Langa
......
......
Sio swala la uoga,Kuogopa ukunguru
Ila bora Kulogwa kuliko kukosa uhuru
Wapi sheikh Mponda,wapi jenerali Komba?
Sera Kali serikali cheza mbali na wajomba
Kimbia,Mitihani imevuja nyie hamjasikia.?
Yanini kusoma huku elimu inanunuliwa.?
Kimbia,NCHI IMESHAUZWA HII HAMNA KUSIKILIZIA,
TANESCO,MADINI hadi AIR TANZANIA
Watoto wa uswazi hawana matumaini
Ndoto za ujambazi sababu ya umasikini
Matapeli wenye shahada kila hatua tatu
Makahaba wa miaka 13

Ngoja niishie hapa ila kama huu wimbo ungetoka 2017 sasahivi tungekuwa tunampelekea chakula segerea.
mwenyezi mungu amlaze anapostahili Amin
 
Langa moja ya wasanii niliowakubali na nitazidi kumuombea huko aliko
R.I.P BRO!

"Chakwake cha kwako,cha kwako cha kwake pamoja wakati wote kama kidole na Pete,sio lazima awe ndugu hata Mtu wa mbali ukiumia anasikia uchungu anakujali kwa kila hali"

"Tenda wema nenda zako atayekulipa Mungu sio unawekeza ulipwe usipolipwa majungu"

-Rafiki batiri hawezi tunza siri,kilemba cha ukoka Nyoka ndumila kuwili--

Uandishi wake wa mistari na tiririka yake ilinikosha sana katika nyimbo zake!

Heshima kwako brother!
R.I.P
 
Chidi benz,na wasanii wote wasioheshimika saiv ipo siku nao watapata heshima nzuri nzuri na sifa kede kede kama Langa.
Sawa-sawa!!

Binadamu walio wengi nadhani ni kama tabia wachache sana watakao kupongeza kwa jambo flani,sifa nyingi utazipata ukisha potea dunia hii, japo ulistahili ukiwa bado hai.

Sikiliza ngoma ya Nikki Mbishi
"Usisubiri"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom