Andaa pesa ya kiwese tu mkuu, ukipata iliyoko safi nikutia mguu tu!
Mmh, ukiachia matangazo at work ambalo sina shida nalo, jaribu kunoa your entrepreneurial skills, mapenzi yaaina ya gari na gharama za uendeshaji wa biashara sioni kama zinatakiwa kuwa tatizo la kiaamuzi kwa mjasiliamali yeyote.
Mkuu, hii ndio gari, cc 2.5, Tdi 3, engine bomba sana hiyo ya dizeli.
Land Rover ni gari imara, hard to break it, lakini spare zipo juu kidogo. Ila ukifunga genuine parts, unasahau kabisa. Sio kama Toyota janjajanja.
Kama ndio unaanza biashara nigekushauri uwe na gari ya pili just incase( kama Suzuku au Toyota); Discovery ni gari nzuri na ngumu. Ila zina mchezo wa kubuma njiani kwa ajili ya vitu vidogo vidogo. kama Sensors, Over heating, Air suspension leakage etc.
Na ni shida kwa Dar (imagine uko mkoani) kupatu fundi and Spare on emergency basis.
All the Best.
I sold mine.
Mkuu, mafuta kama ukilenga engine nzuri utakwenda mpaka 10 Km/Ltr. Lakini ulaji wa mafuta unategemea sana vitu viwili:tell me mkubwa, consumption ya mafuta ilikuwaje? na ilikuwa cc ngapi?
Lita moja ni km 9-10 kwa ile ya cc 3900 ila km engne iko superb haijachoka na parts zake zina operate vzur.. Kwa shuguli za ujasiriamali skushauri kutumia hii gar kwa sababu zifuatazo:
1. Maintainance
Mkuu hii gar mpka ufanye full service nzur gharama yake ni kuanzia 150,000/- kuendelea hapa weka vitu basic tu km filters, oil ya BP ingawa total ni nzur but sio recomended kwa gar hizi.
2. Spare parts zake zinapatikana kwa shida na ni expensive kupita maelezo. Halaf km mkuu mmoja alivodokeza hapo juu swala la sensor ni tatizo ingawa hutegemea na matumiz. Pale Tabata garage moja inaitwa Maximum walipata kuigongesha chini gear box wakiifungua wakaua sensor za gar kwa 60% hawakujua cz washazoea kugongesha za gx100 walipokuja kufunga gar haikuwaka mpka jamaa wa DT Dobie wakaja kuivuta ndo kujua tatizo
3. Kwa mtu unaetaka kutengeneza pesa unahitaji matumiz madogo kwa kadri uwezavyo sasa kwa hii mashine mkuu itakua ni vice versa cz hapa bills zako zitakua juu pengne ukakuta unaifanyia kaz gar tho sio lazima iwe hvo kutegemea na kipato chako ila nahisi unaweza kwenda na choice nyngne na sio Discovery.
Pale kwenye tatizo la kuchemsha inatokana na thermostat inayofungwa kweny rejeta weng hawazifanyii modification ndo mana zinawasumbua ila km ikifanyiwa modification kuchemsha haitkua tatizo la lazima.
All in all hii ni gar nzur sana kwa uimara na comfortability ila inahitaji mfuko wenye afya na sio pesa ya mawazo.
Mkuu, mafuta kama ukilenga engine nzuri utakwenda mpaka 10 Km/Ltr. Lakini ulaji wa mafuta unategemea sana vitu viwili:
1) Ubora wa engine pamoja parts zake kama pump na nozzles
2) uendeshaji wako - ukizingatia ni Auto transmission.
3) maeneno - kama upo milimani tegemea utaendeshea gia kubwa muda mwingi..gari itahitaji power kubwa, more fuel will be consumed.
Issue ya senssors na kuchemsha ni kweli, usipokuwa makini ikianza huo mchezo haitaacha hata kidogo....lazima kuangalia gari kwa makini.
Pia zinatabia ya kuwa KIKOJOZI - leaking oil kama hutakuwa unafuata service na kukagua gari mara kwa mara.
gari gani yaweza kua mbada wa discovery, when it comes to uimara wa gari, stability barabarani and fuel consuption?
Kwa shuguli zako za ujasiriamali i suggest Toyota Hillux 2.4 D4D Vigo hii mashine ni so powerful, consumption nzuri, fast, spare parts available, very durable na ni ngumu/imara.. Pia mafund wake ni wengi.
Tatizo D4 engine huwa zinasumbua sana
Askwambie mtu mkuu wala usisikilize maneno ya mtaan D4 ni engne inayotumia umeme mwing na composition yake sehem kubwa ni electronic tofaut na yale ma engne ya zaman ambayo composition yake kubwa ni mechanic sasa mafund wetu wa mitaan wamekutana na technology mpya inawasumbua ndo wanasingizia labda wew mkuu uniambie hapa kama kweli unazifaham D4 matatizo yake ni nn? D4 na VVTI ni one of the best engine technologies nilizowah kukutana nazo.
Sawa ndio ni nzuri sana ila ni kwa mijini ndio inafaa kwa sababu hautakiwi uchanganye mafuta na wengi hawajui tofauti ya premium na super au regular wanachojua ni petrol wakifika sheli ni kuweka mafuta tu kitu kinachovuruga utaratibu wa hizi injini so ni gharama sna kuzihudumia tofauti na injini nyingine kama 3s au vvti
Hakuna engne ambayo ukiiwekea mafuta mabovu yaliyochakachuliwa haitakuletea matatizo.