Land Cruiser

Wa nyamadyaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2013
Posts
1,178
Reaction score
529
Waungwana habari zenu,
Mwenye kuifahamu gari aina ya land cruiser vx hasa ulaji wa mafuta na matengenezo. Maana yupo ndugu yangu ughaibuni anataka kunitumia hapa nyumbani tanzania, kama ni yagharama sana uwendeshaji wake basi nimwambie aghairishe maana uwezo wangu ni wa mchumia tumbo.
 
Engine ni zile za coaster cc 4500 kazi ni kwako !!
 
hizo zipo kibao mjini utakuwa sio mpya mwambie akutumie Range Rover au Hammers au hata Aston Martin sio mbaya pia akipata Buggati utafaidi zaidi

#zitto
 
funguka kwanza ni model gani ya vx. kuna v8 petrol na V8 diesel kuna amazon inakula lita km 3 tu . kuna gx ya kawaida inakula lita km 8 specify engine na mwaka.
 
Huwa ina matairi manne na moja la akiba huwa linafungwa nyuma ya gari.
Mengi huwa yana rangi nyeusi.
Mara nyingi huwa ni milango mitano.
Lina kioo kikubwa cha mbele.
Lina kelia kwa juu.
Mengi huwa yanasumbua sehemu ile ya kupachikia namba hasa kwa huku nchi za kiafrika.
Ila ni nzuri sana.
Mwambie akuletee tuu.
 
funguka kwanza ni model gani ya vx. kuna v8 petrol na V8 diesel kuna amazon inakula lita km 3 tu . kuna gx ya kawaida inakula lita km 8 specify engine na mwaka.

Mimi sifahamu ya mwaka gani wala kama ya mafuta gani ila ninachojua ni vx na sio amazon ila inafanana muundo.
 
We mwambie akuletee ukiishindwa nicheki tupate chochote hata kwa udalali
 
Sijajua yako ni cc ngapi maana zipo hadi za cc 5700
 
Ndugu nikwamba lazima unapokuja hapa kutaka ushahuri uje na details sisi hatuwezi kuota ukisema land cruiser zipo series nyingi za land cruiser
Kwanza ujue nini unahitaji uje hapa tutakupa jibu sasa mwingine anakuja na jibu la jumla eti inainjini ya costa sasa ukiambiwa hivyo unajua ni Land cruiser gani??Muulize nduguyo akupe series tutakupa details na picha tutakupa!!Karibu!
 

Layman explanation
 

Asante
 
lita 1 kwa km 2. sio mbaya mkuu, nunua tu, utaiweza aisee
 
Spea zake kibao kwa town ukishindwa wapelekee wazee wa ndiooo sioooo aka maccm.kifupi ni gari ya gharama kwa kila kitu ndo maana mtu wa kawaida kumiliki si sana labda awe mstaafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…