Radhia Sweety
Umedai tena kwa sauti kubwa kwamba mimi naleta ushambenga kwa "kiingereza [changu] cha kuungaunga". Sawa. Sijakubishia kwa kuwa wewe mwerevu sana kuliko mimi. Je, lugha niliyotumia kabla ya post hii umeielewa, au nayo nimeungaunga?
Halafu sikuelewi wewe unayejiita jina la mdudu nimchukiaye kuliko hata mbu na mende kwa pamoja, unadiriki kusema mimi ni "p FUNK MAJANI" nimezidiwa na "mibange".
Hivi huyo P Funk Majani unamjua au unamsikia tu? Au wewe ni sawa na wale mazuzu wanaolamba matapishi ya wanahabari uchwara bila hata ya kuyaangalia usalama wake na kujiongezea maradhi?!
P Funk hana haja na wadudu kama wewe mnaoganga njaa. Hata mimi nakuona wewe mpuuzi tu ndio maana hata jina lako sikulishika. Wewe huna tofauti na wale mende wa chooni... Unatembea ukinuka na kusambaza maradhi kibao! Ndio maana kila nikikuona popote pale kazi yangu ni kukukanyaga na kukusigina na jinsi unavyotia kinyaa hata kukuondoa kwa kijiti siwezi. Naishia kumwita hausgeli aje kukuchukua kukutupa na kuosha kiatu changu kwa dettol na kukianika juani. Huniwezi kwa lolote wewe na huyo shangingi mwenzako
Radhia Sweety.
Kama mnafikiri kwamba mimi ni mwanamke mwenzenu kwa kuwa natumia jina hili, hebu waulizeni Mods mimi ni nani kabla ya kuendelea kukurupuka kama nyau aliyefukuzwa jikoni akidokoa mboga ya samaki.
Angalieni nimekaa kwenye hii forum miaka ngapi? Naijua Jamii Forums kabla haijawa Jamii Forums. Enzi hizo ikiwa Jambo Forums kulikuwa na wanachama wachache tulioshirikiana kwa hali na mali. Mlipoingia ninyi makinda ndipo mkaanza siasa zenu za chuki.
Mimi nimekuwa nikimshauri ndugu yangu Joseph Kussaga kudumisha amani na kuachana na hiyo kesi kwani inamdhalilisha.
Kama Mkristo nimetimiza wajibu wangu. Kinachowauma ninyi ni nini? Au mnapenda sana kumwona mdogo wangu Judith aumbuke?
Kama hamjui, Jide aliwahi kufanya kazi Clouds wakati ikiwa pale NIC Investment House, Kitegauchumi, Ghorofa ya 5, ilipoanzia. Lakini Judith aliamua kuendelea na kazi yake ya muziki. Namfahamu Jaydee tangu akiwa anaanza kazi yake ya muziki. Au kinawauma pia ninyi Jaydee akifanikiwa?
Acheni roho zenu hizo za chuki. Jibuni hoja kwa hoja. Mtaheshimika. Matusi yenu ya rejareja wala hayanisumbui.
Sitajisumbua tena kulumbana na mafisadi ninyi. In fact, nawaweka kwenye Ignore List yangu!