GedsellianTz
JF-Expert Member
- Jul 5, 2016
- 1,348
- 1,803
Kuna ndugu wanao share jina la ukoo ila hawa share upendo wala faraja,kuna ndugu asiyependa mtoto wa mama yake mdogo afanikiwe ,pia kuna mama mdogo anayefurahia mtoto wa dada yake kuachika kwenye ndoa ,kuna ndugu wanaochanga michango ya harusi wakati ndugu yao mwingine hana pesa ya matibabu hospitalini.
Kuna rafiki mwenye tija kuliko ndugu ,na kuna ndugu mwenye hila kuliko rafiki ,kwenye maisha ndugu ni yule anayekupa faraja,anayekujali wakati wa shida na raha ,dunia ya sasa imekaukiwa watu wema ni vyema tukaishi kwa upendo na amani.Kuna ndugu anayekufanya rafiki na kuna rafiki anayekufanya ndugu hapo kazi kwako.
Wema na utu huambatana na upendo na kuwa mkweli,palipo na uongo hapana undugu wala urafiki wa kweli sababu uongo ni doa baya sana kwa mtu uko daima mdomoni mwa mpumbavu.Kama una uwezo wa kusaidia ndugu basi saidia kwa upendo na sio kwa matangazo .
Ujanja ni kumfurahisha Mungu na kumkwaza mwanadamu ,jifunze kutoka katika gereza la utumwa wa fikra kwa kujikomba na kujipendekeza kwa ndugu wasio kujali wala kukuthamini sababu kuna rafiki mwenye tija kuliko ndugu .Upendo ni kitu muhimu sana ukiambatana na uzima na afya.
Dawa ya chuki ni upendo na hekima ni kusamehe na kusahau Real family does not come from your blood. It is the people standing beside you when no one else is.
#GedsellianTz