Kwenye hili mnasemaje wadau?

Kwenye hili mnasemaje wadau?

Captain mopao

Senior Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
133
Reaction score
384
Habari wadau, ndugu jamaa na marafiki. Naomba kuwasilisha changamoto hii mnaniambiaje katika hili.

Leo nilienda kijiji fulani nje ya mkoa wa Kanda ya Kati kulikua na shughuli ya ujazaji form za hati za viwanja.

Nilinunua shamba miaka kadhaa iliopita sasa mwaka jana wakaja Jiji kusaminisha na kutupa namba za maeneo utaratibu uliokuwa unatumiwa leo ugawaji wa viwanja naona sio rafiki kwa wananchi sheria ipo hivi kama kiwanja chako au eneo lako lina ukubwa wa square meter 1000 hapo watatoa asilimia 33 ya jiji na asilimia 18 ya barabara kwa hio katika square m 1000 unaweza kiwanja chenye square mia tano au mia sita.

Hilo moja pili kama kiwanja chako ni kikubwa na jirani yako ana kiwanja kidogo wanakata kiwanja chako ili kumfidia jirani yako mwenye kiwanja kidogo lakini huyo jirani atakaeongezewa eneo lako atatakiwa kulipia elfu 5 kwa kila square mita ilioongezeka mfano kuna ndugu mmoja yeye kiwanja chake kilikikua na square m 500 jiji wakakata kiwanja cha mwingine na kumuongezea kipande cha squere 200 zidisha mara 5000 kwa kila square m apo gharama atalipa alfu milion moja ya plot ya niongeza apo bado gharama ya upimaji kodi ya ardhi pesa ya kuandaa hati n.k.

Kwa gharama zote unaweza kupata milioni 2 au zaid sasa mimi shamba langu ni kubwa sana lakini ilitokea njia katikati ya shamba ikawa imegawa yakawa km mashamba mawili lakin moja ni dogo na walivokuja kuhakiki walihakiki km viwanja viwili vioja ni kua wamesema wana kata kiwanja kikubwa ili kufidia kiwnja kidogo ambavyo vyote ni vyangu lakini Ajab wanataka nilipe pesa kwenye hizi square m walizoziongeza kutoka kwenye shamba kubwa.

Pili kwenye hili shamba kubwa lilikua na squere m 7000 wamekata hio asilimia 33 ya jiji na barabara asilimia 18 ndan zimebaki squere m km alfu 3 zote wametaifisha na gharama ya kiwanja kimoja ni milion na point zaid shida ipo hapa hizi pesa inabidi ulipe ndani ya miez mitatu haki ya ardhi ipo wap hapa ndugu yan napata hasira sana haya ukiachana na mimi wakaz wengi wa maeneo hayo maskini wa kutupwa kwa kuwaangalia hawataweza kulipa milion ata ukiwapa miez zaid ya miez mitatu dah ndugu.

Naomba kuuliza hizi sheria za ardhi zinazotumika ni zimetungwa na jiji au ni serikali kuu je tunaweza tukabadili huu mfumo kwa kufanya nini mweyekiti wa eneo husika anapokea malalamiko sana ila lawama anamtupia diwani ambaye hapatikani saana apa tufanyeje wadau au kuna mwenye namba za Lukuvi humu.
 
Mwanza sisi maeneo ya milimani walianza utaratibu huo wananchi wakawafungashia hawataki ata hizo hati mpka leo hawajarudi😆
 
Daaah mkuu sehem gan
Mkonze,nzugun,veyula au wap aise maana hii kitu imenikuta mimi

Nami limenikuta HUKOHUKO mahomanyika ila sikubaliani nalo nilikuwa na eneo la ukubwa wa sqm 3420 Leo napewa ka plot kamoja kenye ukubwa wa sqm 600 ! Kiukweli SI haki
Aisee wanazingua sio kidogo alaf gharama ya malipo ni kubwa na bado wanakupokonya squere m alaf bado ulipie ndan ya miez mitatu ila dah bas tu
 
Back
Top Bottom