Kwenu wabunge wa sasa: Hamna hatimiliki ya majimbo

Kwenu wabunge wa sasa: Hamna hatimiliki ya majimbo

Waridi

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2008
Posts
1,025
Reaction score
174
Waheshimiwa wabunge wa Bunge la JMT na hata wawakilishi wa katika baraza huko Zanzibar. Salamu.

Napenda kwanza kuwakumbusha kwamba sisi wapigakura wenu tulipowachagua hatukuwapa ufalme bali tuliwadhamini tu. Cheo ni dhamana ati.

Tuliwapa muda wa miaka mitano kututumikia. Kama mlifanya vema tutawarudisha Dodoma. Si mmesikia ya Filikunjombe?
Lakini kama mmechemka, kumbuka hamna hati miliki. Acheni kulalamika faulo mnapoona warithi wenu watarajiwa wanaibuka na kupitapita. Kama hukufanya la maana, huponi wimbi la UKAWA!

After all, ninyi wa CCM mwenyekiti wenu taifa amekwisha kuruhusu waweka nia kupitapita. Komredi Kinana hali kadhalika. Kwa hiyo, malalamiko yenu na vitisho vyenu ni kilio cha samaki. Kama mlitaka kutetea nafasi zenu, dawa ilikuwa moja tu; maendeleo kwa wananchi, basi.

Mmesikia akina Mhe. wa jimbo la nanilii, huko Arusha na Manyara?
 
Arusha si yuko Mh. Lema,huyu jamaa anazo mbinu za ajabu na inaelekea anashinda tena.
 
Yaani mimi waliniudhi saana katika suala la katiba mpya. siwezi samehe mbunge yeyote wa nagamba
 
Arusha si yuko Mh. Lema,huyu jamaa anazo mbinu za ajabu na inaelekea anashinda tena.

Hashindi,hana weledi wa kuendelea kuliongoza jimbo kwa kuwa hakuna chochote alichofanya.chadema arusha ina wagombea smart sana Ephata Nanyaro, Noel Olevaroya na wengine wengi ambao kati yao tunategemea chadema ipate mgombea. Siyo tapeli lema.
 
Back
Top Bottom