kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,876
Wilaya ya Rorya ni moja ya wilaya za mkoa Mara iliyo mpakani kabisa na nchi jirani ya kenya. Wilaya hii ina makabila mengi lakini kabila kubwa ni wajaluo ambao pia hupatikana katika mkoa wa Nyanza huko kenya. Kwa kifupi hata makabila mengine wanaoishi katika wilaya hii nao wanajua vzr sana lugha ya kijaluo.
Wilaya hii ina matatizo lukuki na mengine yanazidi kuzaliwa kila kukicha na kimsingi jitihada zinazofanyika kuzikabili ni ndogo sana. Yafuatayo ni baadhi ya matatizo hayo
1. Ukosefu wa chakula wa mara kwa mara (njaa)
Wilaya ya rorya ni kati ya wilaya zinazopata mvua kwa vipindi viwili yaani vuli na masika. Ila kwa miaka ya hivi karibuni wilaya hii imekuwa ikikumbwa na njaa hasa inayosababishwa na ukosefu wa mvua za kutosha uliosababishwa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa. Mwaka huu wakati bei ya vyakula vilipopanda mahindi rorya yaliuzwa 180000 kwa gunia bei iliyokuwa kubwa kuliko popote tanzania.
2. Elimu duni
watoto wanafaulu kutoka form four kwenda form five katika wilaya hii bado ni ndogo sana, hii imesababishwa na wazazi pamoja na walezi kutokufuatilia sana mendeleo ya watoto wao, mazingira magumu hasa unaosabaishwa na umbali wa shule zilipo hasa za sekondari, uchumi duni wa wazazi unaofanya watoto kushindwa hata kupata chakula huko mashuleni, ukosefu wa umeme unawezesha wanafunzi kujisomea na watoto kutokujua umuhimu wa elimu yenyewe.
3. Wanafunzi kuacha shule/kupata mimba na kuolewa
Bila shaka Rorya inaweza kuwa ni moja kati ya wilaya za juu zinazokabiliwa na tatizo la watoto kupata mimba wakiwa primary, watoto kuolewa siku chache baada ya kuhitimu elimu ya msingi na kupata mimba wangali wanafunzi. Shida kubwa hapa ni mila mbovu zinazoambatana na uchezaji wa musiki usiku, jamii kupenda kumaliza matatizo kama ya binti kupewa mimba kienyeji, wazazi kutaka mahari na usimamizi mdogo wa watoto.
4. Uvivu wa kufanya kazi
Wilaya hii vijana wengi utawakuta maneo ya senta wakiwa na radio zao mikononi, wakicheza bao au karata. Wakati mwingine wakibishana kuhusu hili au lile. Yaani kujituma kwa kazi kwao siyo kipaumbele kabisa. Hali ya huku ni tofauti sana na mikoa mingine kama Morogoro au Iringa ambapo vijana hujituma sana kufanya kazi. Kuna mito mizuri tu kama Mto MORI na hata ziwa liko pale laikini ni watu wachache sana wanalima hata bustani maeneo hayo.
5. Uharibifu wa mazingira
Kwakweli wachoma mkaa wameharibu sana mazingira katika wilaya hii, maeno yalikuwa na miti kwasasa hata mtoto mdogo anaweza kwenda kuchunga bila hata shida. Misitu ilikuwepo kando ya mto Mori, au maeneo ya iliyokuwa Ranchi ya pale utegi leo ni mashamba ya watu. Cha ajabu watu hawapandi miti kuchukua nafasi ya ile iliyokatwa
USHAURI KWA WANANCHI
Lazima wananchi waelewe kwamba maendeo ya Rorya yataletwa na wao wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii kubwa sana. Lazima wajue Mheshiwa Rais hakukosea aliposema ni bora watu wasiofanya kazi wafe kuliko kupelekewa chakula cha bure. Kama hamtafanya kazi kwa bidii maendeleo yatakuwa ndoto sana katika wilaya hii. Ndg zangu mtakuwa watumwa na wabeba mizigo katika wilaya yenu.
USHAURI KWA VIONGOZI
Viongozi wetu hasa madiwani wamekosa dira na kwa kweli hawajui hasa nini maana ya kuongoza. Hawana dira, hawana vipaumbele wala agenda, wanafanya vitu kwa mazoea na hawana uchungu na wilaya yao. Ni lazima wapige marufuku mara moja miziki ya kwenye misiba, wachukue hatua za kisheria kwa wazazi wanaoozesha watoto wa kike wakiwa bado wadogo na kuwaripoti polisi wote wanaowapa watoto ujauzito au kuwaoa mapema.
Viongozi wasaidie wananchi kuwa na shughuli za kufanya wakati wa kiangazi, wafundishwe ufugaji wa kuku, samaki, kilimo cha mboga na kilimo cha mazao yanayostahimili ukame. Waanze kuwasaka mara moja wanaochoma mkaa hovyo na kuweka amri ya kila mji kupanda miti pamoja na miti ya matunda.
Mbunge lazima aache mara moja kugawa mchele na ng'ombe kwenye misiba badala yake awatafutie wananchi suluhisho la kudumu ya matatzio yanayowakabili. Ugawaji huu wa mchele unapumbaza wananchi na inalenga tu kujipatia sifa na kura, haina lengo la kukomboa wana Rorya.
Nawashukuru sana na ninaamini huenda kuna viongozi au wananchi walioko humu watanisaidia kueneza injili hii. Zaidi poleni sana kwasababu matokeo ya uchaguzi wa kenya yamekuja kinyume na yale mliyoyatarajia . Aksanteni sana