Kwenu Tanesco na Sekretarieti ya ajira.

Kwenu Tanesco na Sekretarieti ya ajira.

nadori

Member
Joined
Mar 5, 2016
Posts
99
Reaction score
63
Kwanza nichukue fursa hii kuwapongeza kwa kazi mnayoifanya yakulijenga taifa hili.Niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu,Hivi karibuni Sekretarieti ya ajira mliwapangia vituo vya kazi watahiniwa waliofaulu sahili zilizopita yani kutoka kwenye database katika Shirika la umeme Tanesco.Kama ilivyo ada wanaopangiwa vituo vya kazi huchukua barua za kuwatambulisha kwa waajiri katika ofisi ya sekretarieti.Sasa baada ya kuchukua barua hizo vijana wameenda kuripoti katika vituo vyao vya kazi na kitu cha kusikitisha wanapofika wanaambiwa mikataba yao haijafika kutoka makao makuu kwaiyo wamebaki njiapanda.Katika vituo vingine wameambiwa warudi mpaka baada ya wiki mbili na wengine waendelee kusubiri kwa muda usiojulikana.Tunaomba Tanesco najua mpo humu mliangalie hili kwa jicho la huruma kwani kuna watu wametoka Dar wamepangiwa Kigoma ambapo hana hata ndugu na hawezi kurudi alikotoka,Hali ni mbaya kwani mtu alitegemea akifika angeweza kupata posho ya kujikimu na maafisa utumishi hawana majibu ya kuridhisha.
Vijana wanataabika jamani angalieni jinsi ya kuwasaidia.Nimeshindwa jinsi ya kuwa tag Tanesco naomba mnisaidie.
 
Kuwa Mpole Bwana Mkubwa, Swala la Kukamilisha Ajira huchuka Muda Kidogo.. Maana Wanaotoa Check Number sio Tanesco ni Utumishi bado hazina pia.. Kuwa mvumilivu..
 
Kulikuwa na haja gani ya kuwaambia waende moja kwa moja kwenye vituo vyao vya kazi kwanini wasingesubiri wakamilishe taratibu zote ndo wawaambie wakaripoti.
 
Kama umepata ajira tulia. Kwena wengine UDSm walikaa miezi miwili. Naona una hamu sana ya kazi. Ka auna barua utumishi subiri. Kazi umepata
Kulikuwa na haja gani ya kuwaambia waende moja kwa moja kwenye vituo vyao vya kazi kwanini wasingesubiri wakamilishe taratibu zote ndo wawaambie wakaripoti.
 
Kulikuwa na haja gani ya kuwaambia waende moja kwa moja kwenye vituo vyao vya kazi kwanini wasingesubiri wakamilishe taratibu zote ndo wawaambie wakaripoti.

Kuna taratibu za ku report katika kituo cha kazi.. Kwaajili ya Kujanza baadhi ya forms baada ya hapo form ndio zinakuwa processed kwaajili ya kukamilisha ajira yako then unaanza kazi rasmi.

Kuna watu wamesubulia mpaka mieze sita kwahiyo sioni kama tatizo litakuwa kubwa sana.
 
Mbona wa kigoma nimesikia wamepewa favour watume Vyeti kwa Email,iko hivi sasa hivi wanafanya VETTING ya vyeti wengine wameonana na REGIONAL MANAGER wao na wakaambiwa siku ya ku report kazini rasmi ni tar 02,Sept kwa ajili ya mikataba na mishe nyingine mkuu hivo kulingana na gharama za maisha warudi kwanza walipotoka.

Kuna jamaa alipangiwa kituo Taasisi fulani ya serikali mwezi wa 11 ila alianza kazi mwezi Jan wa mwaka mwingine na check no. Ikachelewa sana akaanza pata mshahara baada ya miezi 3 ko uvumilivu Muhimu mkuu kipindi hiki.
 
Uv

Uvumilvu unajua unatokea pale unapokuwa abnormal
 
Ndo hivo uvumilivu Muhimu kwenye mambo mazuri wengi walo report kipindi hiki mpaka sasa hawajasign Mikataba sio TANESCO tu kuna TVLA,TPA wenyewe naskia wapo kwenye vipimo,n.k taratibu huwa si hivyo kama tunavyodhani kama mtu umekaa mtaani miaka 2 unashindwaje kusikilizia mwezi mmoja uone kipi kimetimia na kipi hakijatimia.
 
Back
Top Bottom