Kweli yenye mwanzo yana mwisho nikukumbuka ubabe wa hawa wasanii

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,636
9,856
Kauli hakuna marefu yasiyo name inchi, au yenye mwanzo yana mwisho walioitunga wanastahili pongezi leo mda si mrefu nasikiliza E fm nimesikia wimbo wa nakupenda tu by dudu baya hasa hasa ule mstari unasema

''Wanasema miye mkorofi si mkorofi wananichokoza wao ''

Hapo ndio ikafanya nikumbuke ubabe ya baadhi ya wasanii katika tasnia hii ya Sanaa hapa Tanzania

Dudu baya alisifika ngumi jiwe ukigusa tu umenasa katoa sana vipigo kwa wasanii na mapromota aliogopeka ila sasa hivi kwisha habari imebaki story

Kali pina uyu jamaa alizidi ubabe mpaka ikafikia hatua anasema anataka kwenda mtolea mahali Mr blue du haaaa haaaa dunia ina mambo hii ila sasa hivi kwisha habari yake imebaki story tu

Haya njoo kwa mtarishaji muziki wa pale bongo record P funk majani a. K. a kinywere kimoja uyu jamaa bwana katika miungu watu wanaosikika katika mziki wa bongo flavor leo hii basically naye mda ule alikuwa mungu mtu, wasanii aliwafukuza studio hawajui kuimba na maneno ya dharau juu alitamba kweli kweli na wasanii wote heshima ilikuwa kwa P ila leo kwisha habari yake

Kwaiyo hata ambao tunawasikia leo amin ipo siku watakuwa story tu
 
Jeuri za Majani zilisaidia wasanii wengi mno kuwa kwenye mstari.hata ukiwauliza wasanii wenyewe watakwambia hiyo kitu.

Jamaa alikuwa ni zaidi ya producer..alikuwa kama baba yao kama Huwezi kuimba Huwezi ku-record kwenye studio yake anakusimamia mwanzo mwisho kuanzia ku-record mpaka kupeleka ngoma radio.

Ukitaka kujua hivyo cheki baada ya Majani kupotea na wasanii wake wa bongo record wote wamepotea.
 
Swala la "hakuna marefu yasio na mwisho" haliko tu kwa wasanii,ila lipo kwa kila mtu na kwa kila sekta ni swala la MUDA TU,cha msingi jipange na maisha yako hata wewe hapo unayesoma hapa. Palikuwa na Maradona,Ahmed nejadi,Mike Tyson,R.kelly, Lunyamila, Malota Soma, Rashidi Matumla,Misanya Bingi,Bolo yang,Govinda,Daniel Yona,Yusuph Makamba n.k. Ni muda tu, hakuna atakayedumu milele kwenye kile anachokifanya leo.
 
Kauli hakuna marefu yasiyo name inchi, au yenye mwanzo yana mwisho walioitunga wanastahili pongezi leo mda si mrefu nasikiliza E fm nimesikia wimbo wa nakupenda tu by dudu baya hasa hasa ule mstari unasema

''Wanasema miye mkorofi si mkorofi wananichokoza wao ''

Hapo ndio ikafanya nikumbuke ubabe ya baadhi ya wasanii katika tasnia hii ya Sanaa hapa Tanzania

Dudu baya alisifika ngumi jiwe ukigusa tu umenasa katoa sana vipigo kwa wasanii na mapromota aliogopeka ila sasa hivi kwisha habari imebaki story

Kali pina uyu jamaa alizidi ubabe mpaka ikafikia hatua anasema anataka kwenda mtolea mahali Mr blue du haaaa haaaa dunia ina mambo hii ila sasa hivi kwisha habari yake imebaki story tu

Haya njoo kwa mtarishaji muziki wa pale bongo record P funk majani a. K. a kinywere kimoja uyu jamaa bwana katika miungu watu wanaosikika katika mziki wa bongo flavor leo hii basically naye mda ule alikuwa mungu mtu, wasanii aliwafukuza studio hawajui kuimba na maneno ya dharau juu alitamba kweli kweli na wasanii wote heshima ilikuwa kwa P ila leo kwisha habari yake

Kwaiyo hata ambao tunawasikia leo amin ipo siku watakuwa story tu
his carrier is over like mike,anyone
jordan, tyson,jackson.........
 
Speaking of majani is another case, jamaa bado yuko kwenye industry na kwasasa ni muajiliwa nadhani nliwahi kumuona BASATA kama sio COSOTA, bado anashughulika na mambo ya music but through another door.

Sio mungu mtu tena kama alivyokuwa zamani, now nahisi hata wasiojua kuimba anawatamani ili mradi wana mzuka
 
Ila mpaka sasa bit zake sijaona anayeweza kutengeneza tamu kiasi kile!
Nyingi ukisikiliza zinakinai mapema
 
Kalapina na ubabe wake wote aliishia kusanda kwa Ruge na kutafutiwa fursa ya kuendesha kipindi Clouds Tv. Hebu fikiria image aliyokuwa nayo Pina enzi zile na muangalie sahivi hutaamini, eti sahivi kawa ndio muendesha harakati za kuwasaidia wasanii na wanajamii kuhusu madawa, kweli dunia inazunguka. Halafu nilisikiaga Dudubaya na Kalapina kuna siku walikutana USO kwa USO kikanuka, mashuhuda hebu tupeni ubuyu nini kilihappen kwa hawa watabe
 
mkuu ebu mtake radhi majani......au we unafurahia hii hali ya kila mtu kua msanii?beat hazieleweki,zipo kama hazipo
hakuendekeza njaa,aliiheshimu kazi yake na aliijua thamani ya kazi yake hata kwa kizazi kijacho.leo hii wapi utasikia vitu vtamu na adhimu kama vya majani

NOTE;wacha kumueka kwenye makundi ya kijinga
 
Back
Top Bottom