WILSON MWIJAGE
JF-Expert Member
- May 30, 2011
- 276
- 76
Jana (10.11.2011) katika kipindi cha Idhaa ya kiswahili ya BBC jioni kulikuwa na taarifa kwamba Wazanzibar wapatao 30 hivi wamewasilisha barua yao katika ofisi za umoja wa mataifa (Zanzibar) wakitaka Zanzibar kutokuwa katika Muungano na Tanzania Bara (Tanganyika). Katika barua hiyo wanamuomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (Mooon) kukubali na baadae kidogo kuitambua Zanzibar kama nchi inayojitegemea.
Hii sio mara ya kwanza kufanya hivyo japo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huyo alishawakatalia. Sasa wanasema mara hii atumie busara zaidi kwasababu kuna Wazanzibar wengi nyuma yao wanaowaunga mkono.
Hii sio mara ya kwanza kufanya hivyo japo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huyo alishawakatalia. Sasa wanasema mara hii atumie busara zaidi kwasababu kuna Wazanzibar wengi nyuma yao wanaowaunga mkono.