Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,234
- 1,503
Hii nimeipenda .. soma na hii ..Wataalamu wanatumbia watoto huwa wana-act katika intelligent level baada ya ku-reason kulingana na mazingira na anachokielewa. Majibu ya watoto huwa yanafikirisha ama kushangaza. Juzi juzi nilipiga simu nyumbani nikawa naongea na dogo ana umri wa miaka mitano. Nikamuuliza unafanya nini, akajibu anaangalia mpira. Nikamuuliza nani na nani wanacheza, akajibu Iran na Spain (of course baada ya kuambiwa na mama yake). Nikamuuliza we unashabikia timu gani, akajibu Iran. Nikamuuliza dada yake yuko timu gani, akasema Spain. Nikamuuliza na kaka yako nae anashabikia timu gani, akaniambia hapana kwasababu team ziko mbili tu. Dah! nilicheka sana huku nawaza. Kweli watoto hawapendi maswali ya kijinga.
Hebu tupe kisa kimoja kama ulishawahi kukutana na majibu ya kushangaza ya watoto.
FactWatu wenye akili hawapendi kuzaliana. Hilo ndio tatizo kuu hapa duniani.
Hahahahaaaaaa!!! Hii itakuwa ni rafu. Ngojea nikaangalie kwenye AVR.Watu wenye akili hawapendi kuzaliana. Hilo ndio tatizo kuu hapa duniani.
WIvu ni tatizo jingine .. ila mtoa post anaongelea majibu kwa mtoto yalivyokuwa mazuri.Hayo maswali uliyapanga kabla au ulitaka kuhakikisha kama mke ako iko nyumbani na watoto wakati huo ajachochora.....hiyo ndo ingekua mada kuu wanaume tunao fanyia kazi mbali tutapa tabu sana kipindi hiki
HAHAHAHHAHAHAAA! Nilisha-cheki usalama na Whatsapp video call. Ndo nikapiga simu ya mezani kuongea na wototo. Shauri yako......usipojipanga utapangwa!Hayo maswali uliyapanga kabla au ulitaka kuhakikisha kama mke ako iko nyumbani na watoto wakati huo ajachochora.....hiyo ndo ingekua mada kuu wanaume tunao fanyia kazi mbali tutapa tabu sana kipindi hiki
Hahahaaaa!!!Mwanangu wa miaka 4.5 alinikimbia nikawa namuita na yeye anakimbia tu
Baada ya muda akasimama nikamuuliza wakati nakuita mbona hukusimama akanijibu " Nikiwa nakimbia masikio hayasikii"
Duu nikabaki nacheka
hahaha haha ...kabisaaaWatu wenye akili hawapendi kuzaliana. Hilo ndio tatizo kuu hapa duniani.
savage[emoji1] [emoji1]Amekuja mtoto wa mama etu mdogo nyumbani,,,sasa ni mtundu sana sana yuko pre unit ila hajui kusoma ,,
Sasa anautundu wa maudhi sana,,,nikamkaripia nikamwambia acha utundu,,tulia utundu umekujaa kichwani hamna kitu hapo hujui kusoma wala kuandika,,alichojibu sasa,,akanambia NINGEKUA NAJUA KUSOMA NA KUANDIKA SI NINGEKUA LA SABA,nikawa mdogoo
Uko sahihi mkuu. Ila wakienda shule tu, hapo ndipo wanaharibikiwa. Shule tunawafundisha nini cha kufikiria. Badala ya kuendelea kuwafundisha jinsi ya kufikiria.Hao watoto mkiwakutanisha wote tutashinda kombe la dunia lijalo.
Dar! nimekukubaliUko sahihi mkuu. Ila wakienda shule tu, hapo ndipo wanaharibikiwa. Shule tunawafundisha nini cha kufikiria. Badala ya kuendelea kuwafundisha jinsi ya kufikiria.
Hahahaaaa!! Yaani usijichanganye mbele ya watoto. Hawapepesi!!!!Nyumba ya kupanga nnapoishi kuna jamaa ***** lakini haoneshi ila tunajua!sasa nna dogo wa miaka 5 hivi.siku hiyo gari ya majitaka imekuja kuvuta nikasema kimaskhara tu sijui nani aliejaza choo!
si akamnyooshea jamaa kidole huku anasema yule pale kila saa anaenda kupuu!niliingia ndani spidi kwa kuona aibu