Kuna vijana juzi walipeana adhabu kama mmoja atashindwa kutimiza majukumu waliyowekeana, moja ya adhabu yao ni kuvaa Tshirt na kofia ya CCM kwa siku nzima ama fine ya 100,000/-.
Cha ajabu vijana wengi walikubali kulipa hiyo fine.
ah hahaha haaaa hahaaaa, ni kweli maana sheria haijatafsiri kitu kibaya ni kwa kiasi gani
hivyo yoyote anayeona hajafurahishwa nacho anaweza akashitaki
Porojo ....
Ungetusaidia kama ungetuwekea jibu walilomptia huyo muuliza swali, ili tuweze kufahamu hatua za kuchukuwa pindu tutakapopata huo ujumbe wa kuudhi wa CHAGUA CCM.
Issue sio ubora, issue ni fedha zilizotumiwa kujenga zimetoka wapi?.........Jibu ni Mkopo.......Kama ni mkopo, uliidhinishwa na bunge kama sheria inavyosema?
Jibu ni hapana, kwa nini hazikuidhinishwa? Jibu ni kwamba mikopo ni aina mpya ya UFISADI, no body knows how much kimekopwa, kwa ajili gani na kutoka vyanzo vipi........Deni la taifa sasa lipo kwenye Tsh trilioni 30+. kwa mwendo huu CCM itaikabidhi nchi kwa waliowakopesha muda si mrefu.
kaka wewe unaishi Tanzania ipi? Fanya jaribio chanya, Chagua mkoa wowote ule, kisha chagua kijiwe chochote kile chenye vijana 10 na kuendelea - fika pale anza kujieleza kwamba wewe unatoka Lumumba!! na lengo lako hasa umefika pale kutafuta wanachama wapya wa CCM hasa vijana - Yatakayokupata hapo uje humu utupatie ushuhuda.Porojo ....
Chama kimoja kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 lazima kitachukiwa hata kama kitajitahidi kutenda mema. Watu wangependa waoine mabadiliko. CCM kinaweza kikajinasibu kwa kujenga barabara nyingi za lami, lakini swali zina ubora kiasi gani. Kabla hatujapongeza juhudi hizo za serikali tujiulize, je barabara hizi zimejengwa kwa pesa zetu au kwa mikopo? Kama kwa sasa deni linakaribia trillion 40 kutoka trillioni 7 wakati serikali ikiingia madarakani hatuna sababu kubwa ya kupongeza. Baba akijenga nyumba nyingi kwa fedha ya kukopa kutoka benki watoto wake hawana sababu ya kushangilia kwani iko siku akishindwa kulipa deni zitapigwa mnada. Huwezi kushangilia kujenga nyumba nyingi za kisasa wakati hati za nyumba hizo hunazo. Nyumba ni hati, kama huna hati nyumba hiyo si ya kwako. Tutafakari.
Mngekuwa na akili timamu mngejiuliza kwanini CCM inaendelea kuchaguliwa na watanzania licha ya propaganda zote hizi!kaka wewe unaishi Tanzania ipi? Fanya jaribio chanya, Chagua mkoa wowote ule, kisha chagua kijiwe chochote kile chenye vijana 10 na kuendelea - fika pale anza kujieleza kwamba wewe unatoka Lumumba!! na lengo lako hasa umefika pale kutafuta wanachama wapya wa CCM hasa vijana - Yatakayokupata hapo uje humu utupatie ushuhuda.
Ushauri: nenda ukiwa umevaa helmet kabisa.