Kweli serikali wasanii sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli serikali wasanii sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CPA, Mar 16, 2011.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Kumbe jeshi la polisi kuzuia maandamano walijua serikali itaumbuka, na sio folen. Kwenye huu mkutano wao wa amani uliofanyika leo manzese watu waliohudhuria ni wachache sana, pamoja na kuwepo kwa mrema, mbatia,.. wangeandamana kama walivyopanga cjui wangejitokeza watu wangapi?
   
 2. k

  kayumba JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa wale wanaojua kusoma maandishi ya ukutani washajua kwamba hii ni janja ya kuwazuia Wale wazee wa maandamano huko mkoani (waliobatizwa jina la Wachochezi) hili wakitaka kaandamana Dar wapigwe Stop.

  Na hapo wakikataa, wataambiwa mbona wenzenu tuliwazuia na wakakubali?. TAFAKARI!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  LICHA YA ADUI HATARI ITAKAYOIUA CCM KWA HARAKA ZAIDI NDANI KWA NDANI HIVI KARIBUNI, CHAMA HIKI KIKO MBIONI KUJITWISHA MIZIGO MIPYA KUMBEBA LOWASA NA HASA KUFANYA MAUAJI YA SAUTI PINZANI KISIRI KUSAFISHA NJIA

  Kama uliwahi kufikiria kwamba CHADEMA ndicho adui mkubwa itakayoiua CCM basi kumbe kweli huelewi kabisa siasa za taifa hili zilivyo lakini hivi sasa kundi dogo ndani ya CCM linaloshikilia uhai wa chama hiki kiko mbioni 'KUSAFISHA NJIA KWA NAMNA YOYOTE ILE mmoja wao kushaka dola 2015.

  Kwa wadadisi wa mambo, adui mkubwa zaidi na wa kutisha ajabu tayari yuko chumbani kwao CCM na hivi karibuni italipuka kuliko KINU CHA NYUKLIA CHA JAPAN na kutuma mionzi itakayoifuta kabisa CCM bukia chama cha upinzani namba 4 baada ya NCCR-Mageuzi hapa nchini.

  Kwa kugusia tu kwa uchache; adui namba moja na hatasri mno hadi hivi, kwa haki kabisa kwa misingi ya kichama walichojiwekea, ni kwamba kule Wa-Tanzania Visiwani wanakiona CCM kama Chama kilichowasaliti kushika dola baada ya Mhe Benjamin Mkapa.

  Hakika jambo hili la USALITI WA CCM KWA WATANZANIA VISIWANI ni tishio kubwa hivi sasa ambapo majina zaidi kutoka Bara yaendelea kutajwa KUMRITHI Mhe Kikwete ambaye naye kwanza hata hatima yake bado haiko wazi kwa umma wa Tanzania.Kwa jinsi mambo yalivyo nchini itakavyolipua Naona baada ya CCM kuwatapeli Wa-Tanzania Visiwani nafasi ya kugombea Urais, katika ule mpango wao maalum wa SIASA ZA KUKABIDHIANA UONGOZI WA NCHI KWA ZAMU KWA WATOTO WA WAKUBWA tu Bara na Visiwani.

  Kitendo cha kikundi fulani kujipenyezea fedha haramu kupitia kwa akina Rostam Aziz na Edward Lowasa katika dakika za majeruhi kushawishi maamuzi kumtosa Mhe Salim Ahmed Salim (ambaye alipendwa sana bara na kuaminiwa mno na CCM-Mwalimu Nyerere) kule Dodoma, ndipo jini dume lenye vichwa viwili lilipozaliwa na kuleta salamu za maangamizi kwa hiki chama kilichowahi kupata umaarufu wa miaka mingi sana na kuaminiwa wa wengi nchini.

  Miongoni mwa hizo salamu ni pamoja na (1) Wana-Mtandao badala ya Wana-CCM (ambao nao walikujakugawanyika mbele ya safari na kuwa (i) Wanamtandao Walaji (MAFISADI WA HIVI LEO) na Wanamtandao Waliwa ambao nao mahasibu yao mazito na yanayo nuka mno tutakuja kuyaelezea siku nyingine humu, (2) Wana-CCM Bara ambao lao ni kuwatumia baadhi ya Wana-CCM maswahiba kutoka Visiwani wakiwachezesha kama mchezo wa CHESS au DRAFT KISIASA ili kuzuia Wa-Tanzania wa kawaida Bara na Visiwani kuwa na maamuzi yoyote juu ya nani awaongoze isipokua tu maamuzi yote yatatoka siku zote kwa hii CCM Bara tu kwa sura zima ya Jamhuri yetu ya Muungano Tanzania.

  Sasa kwa ujio wa CHADEMA na kuendelea kupendwa sana kwa chama hiki na azma yake ya KURUDISHA UONGOZI WA NCHI MIKONONI MWA WANANCHI WENYEWE kote Bara na Visiwani, na haya madai Moto Moto ya sisi Vijana kutaka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kote ndani ya taifa letu tayari zimekua ni mwiba mchungu katika ngozi ya kikundi hiki cha WAJANJA WACHACHE Wana-CCM Bara ambao mpaka hivi sasa, kwa mujibu wa habari nyeti za ndani sana chumbani mwao, kila ramani ya kisiasa wanalolichora linagoma kabisa, fedha walizokwisha wekeza kwenye juhudi hizi zote Bara na Visiwani zakumbwa na hatari za wazi mno na migawanyiko kuongezeka kila kukicha kati yao.

  Hata nako ndani ya kikundi hicho cha hao Wajanja wachache Wana-CCM kumeibuka nako Migawanyiko mikali ya KI-KANDA kwa namna ambayo hata juhudi gani zifanyike hakuwezekani kupatanishwa kitu hata wakafanya kazi kwa pamoja.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya CCM katika ujumla wake, hali si shwari hata kidogo mle!! Wapo hata wale ambao, kwa ufinyu tu wa mawazo, wamefikia mahala wamependekeza MAJINA 15 ya baadhi ya watu mashuhuri na tishio kwa maslahi yao KUUAUA. Lini wauawe na kwa MTINDO GANI usioweza kuleta tafrani kwa kile wanachokiita 'Tishio la Nguvu ya Umma' kutokuweza kuwakumba.

  Japo tatizo letu Wa-Tanzania tuliowengi ni mpaka tushikishwe jambo kiganjani ndio tuamini na wakati mwingine kugutuka kukiwa kumechelewa sana, miongoni mwa HAYO MAVUNO YA MIKONO YA KI-SHETANI tayari wameorodheshwa baadhi ya vinara wa kupinga madhambi ya CCM kwa njia mbali mbali nchini.

  Kati ya watu wanaolengwa wamo (i) baadha ya viongozi tishio kwa kinyang'anyiro cha kiti cha urais 2015 waliomo ndani na nje ya hicho kikundi cha Rostam Aziz na Edward Lowasa. Pia, (ii) wapo baddhi ya viongozi wa serikali za wanafunzi nchini, (iii) baadha ya Wana-JF ambao wametajwa kama 'wakorofi na waharibifu', (iii) baadhi ya viongozi wa dini katika kanda fulani ambao wameelezewa kuwa na 'vinywa pana' na kuonekana kukisaidia CDM, (iv) wafanyabiashara wanaohofiwa kukifadhili CHADEMA hivi sasa na (v) na baadhi Wanataaluma wanaoonekana kujitolea kukisaidia CDM ki-mikakati ambayo hadi sasa yaelezewa KUKIDHOOFISHA MNO hiki chama tawala.

  Sasa chama hiki chaonekana kubuni (1) mkakati mpya wa UONZOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kukabidhiwa kwa zamu ile ile ila safari hii ni NDANI KWA NDANI TANZANIA BARA na vile vile ni (2) kwa KUZINGATIA AMA URAFIKI, UJIRANI AU UDINI kufanya hivyo.

  Hata hivyo nako mambo si yenyewe baada ya wale wafadhali wa Uarabuni (Libya, Misri na Iran) nazo kukumbwa na matatizo kibao, yale yanayoendelea na yale ambayo yatalipukia kwao miezi michache ijayo; kikundi hiki ndani ya CCM kimechanganyikiwa kupindukia kwani kwani ufadhili wao hauna uhakika tena huku wananchi tukiendelea kulishikilia bando DOWANS na mianya mingine itakayotumika kuchota kodi zetu kuyatekelezea haya yote.

  Dawa ya yote haya wanayopangwa kutekelezwa kwa mikono ya giza ni (1) kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anageuka kuwa mlinzi wa mwenzie dhidi ya juhudi hizi hatari, (2) kusimama kidete kwa KUSISITIZA Katiba Mpya ya Wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi kupitishwa Bungeni mwezi ujao, (3) kuendelea kuhakikisha kwamba UTEUZI WA JOHN MIMOSE CHEYO kushika tena ile kamati kule bungeni haiwi tena kichochoro tena cha Mafisadi kujichotea fedha kununulia kura na kutekelezea mambo machafu huku Cheyo akijifanya hajaona kitu kwenye vitabu vyetu!!
   
Loading...