Kweli Ndoa yataka Moyo.....

true_diva

Member
Jan 5, 2013
53
25
Ndugu zanguni yamenikuta na naomba ushauri wenu,Mimi ninaishi na mume wangu yapata miaka miwili sasa,nina mpenda sana Mume wangu na ninaamini kuwa naye ananipenda pia.Ila kuna tatizo linanisumbua sana juu yake ambalo linanipa wasiwasi kiasi kwamba nashindwa kuelewa hatma ya mahusiano yetu ya ndoa kwa maana ya kwamba nahofia yasije yakaingia shubiri na ile imani nlionayo juu yake ikateteleka.Ni hivi kabla ya kunioa mimi aliwahi kuwa na mahusiano na wanawake wengine ila mwanamke wa mwisho ambaye aliachana nae amekua akiendelea kuwasiliana na mume wangu na kila ninapohoji juu ya hilo Mume wangu hunijibu kuwa hauna kitu kinachoendelea baina yetu ni rafiki yangu tu wakawaida na hana shida yoyote na sisi kwanza huwa anapiga simu na kutuma meseji za kutujulia hali,anyways nimejitahidi sana kuwa na mtizamo chanya na kuuambia moyo wangu uamini hivyo.Ila siku zinavyokwenda nikaona mazoea yanakua sio mazuri kwa maana wakati mwingine humpigia simu ana hutuma meseji humueleza mume wangu kuwa amemmiss sana na anataka kuonana nae na vitu kama hivyo.Nlimwambia mume wangu mawasiliano na huyo mpenzi wako wa zamani hayanibariki hata kidogo naomba uwe na mipaka na ikibidi uache kwa maana yananiumiza mimi zaidi,aliniahidi kufanya hivyo na kweli kwa kipindi fulani kazi ilipungua ila sasa leo ametuma tweets kuhusu mume wangu kwenye mtandao wa twitter kitu ambacho kimeniuma maana anaeleza jinsi anavyofurahia tendo la ndoa na mume wangu na baada ya kuliona hilo nkampigia mume waqngu kumweleza akaniambia atampigia simu kumsema juu ya hilo na kumuonya.Badala yake kilichotokea yule mwanamke alituma tweets za kunitukana na kunidhalilisha mimi kitu ambacho kinaniuma sana kwa maana mume wangu anasema yule mwanamke ni rafiki mzuri tu na hana shida hata kidogo.Nisaidieni ushauri ndugu zangu je niendelee kuvumilia hayo yote yanayojitokeza na kuamini maneno ya mume wangu kuwa huyo mwanamke hana shida na sisi ama nifanyenye?Naomba ushauri wenu katika hili.....
 
hakuna urafiki wa mwanaume na mwanamke ambaye alikuwa X wake,lazima wanado.Mmeo lazima akufiche.Na inawezekana yule demu anapewa kichwa na mme wako,kwa nini akutukane?ila vumilia ndo ndoa hiyo.
 
Ukiona hivyo jua mme wako kakuchoka au kuna vitu adimu alikuwa akifanyiwa na huyo mpenzi wake sasa kavimiss ndiomaana anaamua kuvifuata huko,ushauri wangu kaanaye tena muhakikishie aacahane naye otherwise unalifikisha kwa wazazi.
 
Urafiki na ex?..damn!
Kwa sasa naomba niseme tu ' a house divided against itself cannot stand'
Mwambie mumeo bygones are just bygones...hapo unaibiwa mchana kweupe!
Ni mawili ama uamue kushare na wazamani au upiganie ndoa yako...
 
mnh hilo limume lako haliwezi kufanya maamuzi magumu,huku anataka na kule anataka....huyo mwanamke naye is either anataka kurudisha majeshi ama wameshakulana kisiri siri,hapo cha kufanya ni kuachana na mumeo,....magonjwa siku hizi ni mengi mamiii just cut the ties waachie wajinafasi.......obvious ungekuwa first priority huyu mume asingekuwa anacheza na psychology yako na kukuumiza
 
binti, hakuna cha ushuari hapo, uamue ili mumeo aamue

hiyo ni vita kati ya wewe na huyo dada ambaye anaamini wewe ulimpora penzi, na huyo mumeo ni -----... si heshima hata kidogo kuruhusu mtu wa nje kutawala au kuingilia ndoa yako, huyo ----- alitakiwa apige stop huo ujinga zamani sana, hata kama anendelea nae, lakini alitakiwa awe ameweka mipaka kati upuuzi wake na ndoa yake

una maamuzi mawili tu, kuanza mbele, au kupambana, lakini kwenye kupamba kama mumeo yupo upande wa pili, ujue huna chako.

siku hizi watu wana-share ndoa hdi 15 years.... kama umekubali hilo, basi jiandae kuwa na watoto wengi tu wengine uliowazaa na wengine wa huyo dada nk

The bottom line is... MUMEO NI ----- NA HAJUI NDOA, ALITAKIWA AWEKE MIPAKa, HUYO DADA KESHAMGEUZA MUMEO JOYCE WOWOWO
 
binti, hakuna cha ushuari
hapo, uamue ili mumeo aamue

hiyo ni vita kati ya wewe na huyo dada ambaye anaamini wewe ulimpora
penzi, na huyo mumeo ni -----... si heshima hata kidogo kuruhusu mtu wa
nje kutawala au kuingilia ndoa yako, huyo ----- alitakiwa apige stop huo
ujinga zamani sana, hata kama anendelea nae, lakini alitakiwa awe
ameweka mipaka kati upuuzi wake na ndoa yake

una maamuzi mawili tu, kuanza mbele, au kupambana, lakini kwenye kupamba
kama mumeo yupo upande wa pili, ujue huna chako.

siku hizi watu wana-share ndoa hdi 15 years.... kama umekubali hilo,
basi jiandae kuwa na watoto wengi tu wengine uliowazaa na wengine wa
huyo dada nk

The bottom line is... MUMEO NI ----- NA HAJUI NDOA, ALITAKIWA AWEKE
MIPAKA YA UPUUZI NA UJANA KWANZA

nashukuru kwa ushauri wako ntaufanyia kazi
 
Funga na kuomba ndio njia pekee kama unaipenda ndoa yako.
Mdada anaharibu ndoa yako
Mumeo anaruhusu
Hakuna unachoweza fanya zaidi ya kusali kuiombea ndoa yako.

nashukuru mpendwa sitakata tamaa kwny maombi....moyo wangu unateseka sana
 
nataka kubaki maana nampenda sana mume wangu kutoka moyoni[/QUOT

Sasa sikia,unachotakiwa kukifanya ni kigumu lakini ni dawa kubwa sana. Puuza vitimbi,maruerue na makorokocho ya mume wako kwa huyo mwanamke mwingine. Achana na kufuatilia mawasiliano ya mume wako na huyo mwanamke mwingine.

Ni hivi,binaadamu ameumbwa kama kiumbe mpenda sifa.Unapomfuatilia na kumhojihoji mumeo ndipo yeye anapoongeza manjonjo ya mawasiliano na huyo mwingine ili akuumize zaidi. Unamfanya ajidai kuwa 'kwake umefika' na hauna jinsi. Anavimba bichwa. Anakudharau. Anakupuuza.

Mpuuze naye aone anachokifanya ni upuuzi. Lakini,siku moja moja chachamaa na utishie hata kumlazimisha kupima afya. Atafyata mkia. Ndoa yako itakuwa salama.

Fanya hivyo uone
 
cheza na maisha kama unavyochezea shilingi chooni,mie nilipima VVU once in my life and i vowed not to do it again.........wanaume walivyojaaa waiiiii:tape2:
 
nataka kubaki maana nampenda
sana mume wangu kutoka moyoni[/QUOT

Sasa sikia,unachotakiwa kkufanya ni kigumu lakini ni dawa kubwa sana.
Puuza vitimbi,maruerue na makorokocho ya mume wako kwa huyo mwanamke
mwingine. Achana na kufuatilia mawasiliano ya mume wako na huyo mwanamke
mwingine.

Ni hivi,binaadamu ameumbwa kama kiumbe mpenda sifa.Unapomfuatilia na
kumhojihoji mumeo ndipo yeye anapoongeza manjonjo ya mawasiliano na huyo
mwingine ili akuumize zaidi. Unamfanya ajidai kuwa 'kwake umefika' na
hauna jinsi. Anavimba bichwa. Anakudharau. Anakupuuza.

Mpuuze naye aone anachokifanya ni upuuzi. Lakini,siku moja moja
chachamaa na utishie hata kumlazimisha kupima afya. Atafyata mkia. Ndoa
yako itakuwa salama.

Fanya hivyo uone

asante sana kaka Petro kwa ushauri mzuri na wenye changamoto nyingi nitajitahidi kadiri niwezavyo kuyatekeleza hayo hatua kwa hatua na siku bada ya siku,ila ukwl ni kwamba my heart is dying inside
 
Back
Top Bottom