KWELI MASHABIKI WA NCHI HATUJUI MPIRA

Joined
Oct 18, 2026
Posts
31
Reaction score
30
WANAO SEMA MANQOBA AONDOKE HAWAJUI MPIRA!

Nisameheeni kwa kusema ukweli mchungu.

Mtu anayesema Manqoba Mngqithi aondoke Yanga hajawahi kukaa hata dakika moja darasani kujifunza mpira wa kisasa.

Mnatafuta matokeo ya instant kama miaka ya 2010. Mpira wa 2026 sio hivyo.

ANGALIA FACTS, SIO HISIA:

1. Yanga ya Manqoba ina xG kubwa kuliko Yanga yoyote ya misimu 3 iliyopita. Maana yake tunatengeneza nafasi nyingi zaidi, goli linakuja tu.

2. Pressing yake ndio bora NBC. Hakuna timu inayowin mipira mingi final third kama Yanga. Hiyo ndio mpira wa Ulaya.

3. Anacheza na mfumo, sio na majina. Leo Pacôme hayupo? System inabaki ile ile. Hapo ndipo unajua kocha ni bora.

4. Mtu aliyemfundisha Pitso, aliyecheza na Mamelodi kwa miaka 10, unataka umfundishe wewe wa Kibaigwa uliyefeli hata kufundisha timu ya mtaani?

Tatizo letu mashabiki wa Yanga ni moja: TUNATAKA KUSHINDA KILA MECHI 5-0. Tukishinda 1-0 tunasema kocha mbovu.

Real Madrid ya Ancelotti ilishinda Champions League kwa kushinda 1-0 nyingi. Mpira ni matokeo + mchakato.

Manqoba anajenga mchakato. Matokeo yatakuja yenyewe na yata-baki kwa miaka.

Kama bado unasema aondoke, tafadhali rudi kuangalia soka la mtaa kwanza. Yanga ya sasa ni ya watu wanaoelewa mpira.

*STAY. PROFESA MANQOBA STAY💚💚💛
 
Mfano mzuli no huyu kocha wa Simba Steve Barker amekuta Haina presha inacheza ikishinda saw ikifungwa barid ty lakin kapewa mda dada anaonyesha kitu
Ewaaah! Sasa unaona jinsi Simba na Yanga walivyo, ehh!

Akili za viongozi wa hizi timu ukiwa mfuatiliaji lazima utaijua tu. Na unaweza kutabiri kitakachotokea.
 
Unalipwa kiasi gani kumtetea tapeli Manqoba mpigwa miti?

Anatimuliwa tu we subiri utaona.
 
Tunajiuliza ile Yanga iliyoanza msimu iko wapi hatuioni. Kuna wakati Yanga tulikuwa na changamoto ya umaliziaji, ila kwa sasa timu yote haieleweki. Kikubwa tuombe Dickson Job na Mzize warejee mapema.
Kwa uchezaji huu, hata kombe la ligi tusahau.
 
Mpira wa Tanzania unasiasa nyingi Yani influencers wakiamua kocha aondoke anaondoka kweli
Sio influecers, ni uhalisia. Yanga ilianza vizuri preseason, na game chache za mwanzo, baada ya hapo timu imepotea. Mechi za club bingwa nusura tutoke mzunguko wa kwanza, mechi na Simba- sikumbuki Yanga iliyoonyesha kiwango kibovu namna ile.
Kama kuna ishu kati ya kocha na wachezaji zifanyiwe kazi.
 
Ni kocha mzuri ila ukubali ukatae Yanga tunashida ya fitness coach

Wachezaji yanga sasa karibia kila mechi mchezaji anaumia hii ni hawako fiti jaribu kucheki timbeili la kangwanda alipofika tu na sasa
 
Umesema
"1. Yanga ya Manqoba ina xG kubwa kuliko Yanga yoyote ya misimu 3 iliyopita. Maana yake tunatengeneza nafasi nyingi zaidi, goli linakuja tu." Hili nakataa

Kwa mechi za mwanzoni mwa msimu ilikuwa hivyo, Ila kadri siku zinavyoenda ndipo tunaona timu inacheza mpira wa hovyo na magoli yanakuwa ya jitihada za wachezaji ama makosa ya timu pinzani.

"2. Pressing yake ndio bora NBC. Hakuna timu inayowin mipira mingi final third kama Yanga. Hiyo ndio mpira wa Ulaya." Hili pia nakataa
Narudia tena laiti kama hatukuona mechi ya Geita, Gaborone na Simba basi tungekubali unachosema kuhusu hiyo pressing. Mechi na Simba ndio aibu tupu yaani Yanga ndio iliyokuwa inafanyiwa pressing na muda wote wanashambuliwa tu, wakipata mpira hata haichukui dakika wamepoteza.

3. Anacheza na mfumo, sio na majina. Leo Pacôme hayupo? System inabaki ile ile. Hapo ndipo unajua kocha ni bora. Hili pia sio kweli.
Kwa mtu anayeangalia mpira ni ngumu kukubaliana na haya maelezo yako, ingekuwa anacheza na mfumo basi tungekuwa tunaona kwenye sub timu inakuwa imara zaidi. Ila kila akifanya sub timu ndio inaelemewa zaidi, maanake hajui hata anachopaswa kukifanya. Tuliona kwa watangulizi wake kama Nabi, Gamondi na Miloud kuwa Yanga kipindi cha pili wanakuwa bora zaidi kwanzia kimbinu, kiufundi na kiutimamu wa mwili na hadi wapinzani walikuwa wanajua hili. Lakini chini ya kocha, Yanga kipindi cha pili ndio inakuwa hovyo zaidi na kutepeta. Ukibisha ninaweza kukupa stats za vipindi vya pili uone Yanga ya huyu Manqoba ilivyokuwa unga kipindi cha pili.

Klabu bingwa kuna timu zenye ubora na viwango kuizidi Simba, Gaborone na Geita Gold sasa kama hizo timu za kawaida zimemtoa jasho huko makundi si atapuyanga?
 

Ndy timu ambayo imetengeneza chance nyingi ligi kuu sor far
 
Ndy timu ambayo imetengeneza chance nyingi ligi kuu sor far
Matokeo hayahesabiwi kwa idadi ya chance ulizotengeneza bali umezitumiaje hizo chances. Kule Botswana wale Gaborone walipata nafasi moja na ikawa goli, iliweza kutofautisha score board kipindi cha kwanza.
 

Lila mechi Ina plan take huwezi kucheza na simba alaf ukatymia game plan ya ulivyocheza na jkt tanzania
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…