Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magulumangu, Jan 22, 2011.

 1. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nilitamani sikia,kwaheri tokea kwako,
  Japo ulikuwa malkia,shambani hekima kwako,
  umasikini nasikia,ulitoa uhai kwako,
  Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,

  Amani ulihubiri,fisadi wamepokonya,
  ungesema mahafari,sio hasi ningefanya,
  lako juu kaburi,mshumaa ulo nyanya,
  Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,

  sipitali kuchelewa,kunipenda uliwahi,
  mdomoni yalinenwa,kabla ya ile subuhi,
  ni kipindupindu hewa,walisema asubuhi,
  kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,


  Angekuwa mama salma, tume huru ingeundwa,
  wangeenda alabama,uhai wake okolewa,
  mindege dalisalama,radio ingetolewa,
  Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,


  Cha kujivunia sina,zaidi ya yale mapenzi,
  maneno yako si hina, kufutika kama tenzi,
  sasa nimeyaona,ulonichangulia wangu mwenzi,
  kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,

  Wivu daima ulija,kama alo mungu kwetu,
  ulimuonya hata shija,husu sisi chama chetu,
  akakuona wa kuja,kwa kujiona yeye chatu,
  Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,

  Mwangaza ulikuwa,giza lilipotanda,
  mkate si uliliwa,kila kitu kimepanda,
  wako huko ihumwa,bajeti iko kitunda,
  Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,

  Baba pia ateseka, kwa nini ulimwacha,
  ile ahadi mulitaka,timie kila kukicha,
  kukufata anataka,anaogopa wale mapacha.
  kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,870
  Likes Received: 83,348
  Trophy Points: 280
  Una kipaji cha hali ya juu kwenye fani ya hii ya mashairi. Hongera sana
   
 3. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante babu yangu,mie nitakusabahi,
  ile ahadi ya kwangu,kamwe kuja itawahi,
  uchakachuaji si wangu,ni chama kilichotuwahi,
  Babu njoo butiama,wa Taifa lipozikwa,


  Alienda nacho chama,swali kwa watanzania,
  nimebakizwa chadema,kafu iko nalialia,
  tielopi ya mrema,yudipi nacho chalia,
  babu njoo butiama,wa Taifa lipozikwa,

  Arusha nayo mewaka,imeifuata musoma,
  pilipili mwathirika,kudai haki kiama,
  kweli niwamepigika,hata kufa twaungama,
  Babu njoo Butiama,wa taifa lipozikwa,

  Nisalimie hapo moi,ukimuona dokta slaa,
  mpe japo kikoi,dokta asiwe na butwaa,
  mie mlalahoi,yeye ndo yangu slaa,
  Babu njoo butiama,wa taifa lipolala,

  Namchukia makamba,kikwete na chao chama,
  kinaongozwa na salma,ridhiwani naye kiama,
  wapo kama kima,wamekigawana chama,
  Babu njoo Butiama,wa taifa lipozikwa,
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Si mchezo nyie ndo kwetu kule mnaitwa manju!!!:shock:
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
Loading...