Tulishajua hata kabla mkutano haujafanyika. Hawana watu mwanza mjini inabidi wadundulize. Kwanza mkutano gani wa serikali unavaliwa jembe na nyundo? Ni dhahiri walisafirishwa ili angalau kuwe na audience na haswa ndiyo lengo la kushehesha na ngoma za kienyeji.
Watu wa Mwanza haswa mnaosafirishwa na malori. Memjizira na kukosa tumaini kiasi gani hadi kuridhika na maisha hayo? Mmedharaulika kiasi gani kupandishwa malori badala hata ya kuwalipia nauli za bus? Ni kwamba hamna nguo za kuvaa hadi mvishwe jembe na nyundo ama mlindanganywa ni sare? Mnajua tofauti ya ziara za kiserikali na za kichama cha hao viongozi wenu? Ninajua hamwezi kulaumiwa kwa sababu ccm ni chama gandamizi kinachoendeshwa kwa vitisho kwamba ukiwa mwanachama, kama hukubaliani nao utakiona cha moto.
Najua ccm imeua wengi waliotofautiana na nia ovu ndani ya viongozi wa chama hicho. Lakini hawatawaua wote!. Kataeni kutumikishwa. Mnahitaji kuishi maisha huru na si utumwa!.
Jinsi ccm inavyowatishia haina tofauti na ISIS inavyoua watu hadharani na kuwatundika vichwa ili kuwatisha wengine. Ndivyo ukatili wa ccm inavyofanya mchana kweupe ili wengine muogope.
Nadhani sasa ni muda muafaka wanaharakati kwa umoja wao, wafanye crush program ya kufundisha elimu ya uraia na haki za raia dhidi ya wajibu wa serikali. Hali hii inatafsiri nyingi sana!. Poleni ndugu zangu wana ccm mnaotumikishwa kwa sababu ya umaskini na uelewa mdogo. Huo ndio mtaji wa ccm ilyobaki nao. LAKINI YANA MWISHO!.