Nimemsikia mh. Livingstone akihojiwa akasema anashangaa mama ntilie kuwa na laini nne wakati yeye ni mbunge na ana laini moja, akasema tuishi kulingana na kipato, je kwa kauli hiyo amezingatia maisha halisi ya mtanzania?
Mh. Lusinde, kuwa na laini nne, si kuongeza matumizi! wanaofanya hivyo wanataka kubana matumizi. Kwa taarifa yako ukimpigia mwenye laini ya tigo kwa tigo, gharama ni nafuu zaidi kuliko kutumia laini tofauti hivyo hivyo kwa laini nyingine. Ila kwako wewe mwenye kipato "kikubwa" ndiye usiyeliona hilo!