Kweli ananipenda au ananizingua?

young lideko

Member
Joined
May 28, 2020
Posts
42
Reaction score
50
Ngugu zangu naombeni ushauri,

Mwaka mmoja uliopita nilianzisha mahusiano na bongo mmoja hivi, ukweli alipenda kwa dhati na nikajivunia kua nae. Lakini kuna muda fulani alikuwa ananiuliza kwamba je, nitamuoa?

Ukweli swali hilo lilikuwa linaniumiza sana kichwa, kwani mimi sijapanga kuoa halafu yeye anadai ndoa. kwaiyo nikawa namrusharusha tu na maisha yakawa yanaenda tu.

Lakini kuna siku aliniita na kuniambia ameshatolewa barua na anatarajia kuolewa. Ilichukua takriban wiki mbili akili yangu kukaa sawa, maana nampenda sana mwankemke huyo.

Ilifikia hatua chakula nakiona hakina ladha, sina hamu ya kula, usingizi sipati mpaka nikapungua mwili.

Lakin mbali na yote hayo bado alinionyesha upendo na mpaka gheto anakuja, na alikuwa ananiambia nisiwaze chochote kwani ananipenda sana na amefanya hivyo kwa ajili ya maslahi tu kwan huyo jamaa anakipato kidogo tofaut na mimi.

Ndoa ishapita bado nipo nae, geto anakuja na bado ananiambia ananipenda japokuwa tangu kuolewa kwake kwa kiasi fulani mahusiano yetu yana fifia.

Mana tutagombana mara kwa mara lakini bado tupo. Pia naweza kusema kwa sasa tunaishi kama mazoea tu. maana na mimi nishakata tamaa ya kuwa nae tena japokuw nipo nae.

Naombeni ushauri, hivi ni kweli kuna mapenzi hapa?
 
Mke wa mtu ni sumu waa waaa usijaribu chombeza waaa waaa yatakuja yakukute waaa waaa usiyoyategemea...
Kaka imeshapita hiyo la msingi nawe tafuta mamayeyo moja uweke ndani, tuelewe wanawake kila siku wanatongozwa anzia nyumbani kwao, barabarani, shambazi, kazini...nk
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…