kuna sababu nyingi kaka ila kutumia simu yako kama reference hizi hapa ni sababu kuu.
1.hardware za wp ni nzuri
pengine hio 512mb unaiona ndogo lakini hujui ni jinsi gani processor yako na gpu nguvu yake.
processor- krait 300 1.2ghz dual core
gpu ni adreno 305
krait 300 imetumika kwenye s4, htc one, xperia z, moto x nk sema wao wamekuzidi clock speed ila ni same cpu. na adreno 305 pia sio mbaya sana ni gpu nzuri. hizo y530 au y300 zimeachwa mbali sana kwenye cpu na gpu.
kukupa proof zaidi hizi wp za bei rahisi zinakubali technology ya quickcharge ambayo ipo kwenye highend za android kama galaxy note 4. nachaji lumia 620 yangu kwa kama dk30 tu. kwanini inakubali? sababu zinashare same cpu ya krait. nilijaribu kwenye p7 na phantom z mini ilikuwa inajaa pole pole sababu hardware sizo.
2.fragmentation na optimization
sababu microsoft analimit hardware zinazotumika anakuwa na control na os na pia haruhusu manufacture kubadili wp hivyo same experience unaipata kuanzia simu za bei rahisi hadi za bei ghali.
kwenye android stori ni nyengine kila mtu anamodify anavyotaka yeye kuna touchwiz, kuna sense kuna emotion ui mara sjui miui nk kuna qualcom, wengine mediatek, wengine tegra wengine kirin nk ilimradi kila mtu na kitu chake. mwisho wa siku google anashindwa ku optimize android kwa kila siku na kuishia ku lag na kuwa slow.
kama unataka atleast upate android iliokuwa faster inabidi utafute android ambayo sio ya google (aosp (android open source project)), hapa utapata rom kama cyanogen na wenzake.
kama huwezi kuishi bila google then atleast tafuta simu yenye stock android au inayokaribia kama vile moto e, moto g nk
3.nature ya operating system
abdroid yenyewe imekuwa designed iwe na true multitasking hivyo app zinakaa chini kwa chini na kula ram ya simu, kwa simu za 512mb hapa ndio majanga yanapoanzia na mwisho wa siku zinalag. wp haina true multitasking ukitoka kwenye app inapause then ukiingia tena inaresume ila hii nayo pia ina udhaifu wake, mfano huwezi kudownload kitu background kama vile movie hadi app iwe umeifungua.