Kwanini wengi wamekimbilia Windows 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wengi wamekimbilia Windows 7

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Sep 6, 2010.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  kwanini uchague Windows 7


  [​IMG]Microsoft wameweza kuuza nakala zipatazo milioni 150 million za Windows 7 ndani ya miezsi kadhaa tangia iingie dukaniĀ–Hii imewawezesha au kuifanya windows 7 kuweka historia katika mauzo ya kampuni hiyo tangu waanze kutoa au kuuza hizi operating systems.Kinyume chake,Vista ilionekana kuwaboa watu na kuwafanya wafikirie mkabala wa microsoft,binafsi nilikuwa muathirika mmoja wapo,kwani nilikuwa nimetokea kutoipenda vista hata kidogo.
  Kuna baadhi yetu tulibakia kwenye Vista ni kwasababu tu pindi ununuapo kompyuta mpya huja na nakala ya Vista hii hukufanya kutokuwa na la kufanya kwani sio tu kutokana na gharama bali pia kwa kipindi kile Vista ndio ilikuwa mtawala pekee mkuu ukiondoa XP.
  Ahsante kwa Windows 7,sio tu imekuja kutoondoa toka kwenye matatizo ya Vista bali imesaidia kurahisisha matumizi ya kompyuta hata kwa watu wasio na ufahamu mkubwa wa kompyuta kinyume na ilivyokuwa kwenye Vista.Kama munakumbuka kipindi kile tunatumia Vista kila baada ya siku kadhaa unaambiwa kompyuta yako haina nafasi ya kutosha,kila ukijitahisi kusafisha,wapi.Windows 7 imejitahidi kuja na mpangilio mzuri wa mafaili,mambo ya usalama,kuondoa mauchafu yasiyo takiwa,urahisi wa kuhifanya mafaili yako pia muonekano unaovutia na kutamanisha.
  Baada ya kuona hayo kwa muhtasari,sasa tuangalie nini kunako kwenye hii Windows 7?

  1.Mpangilio wa mafaili

  Hii ni kitu ambacho binafsi kimetokea kunivutia sana kwenye Windows 7,imeweza kuondoa matatizo yaliyokuwa kwenye Windows Vista ambapo ulikuwa unatumia miaka kama sio karne kutafuta kitu kimoja tu.Kwenye Windows 7,ubadilishaji wa muonekano au mpangilkio wa mafaili umekuwa rahisi zaidi,ni mwendo wa kubonyeza mara moja tu kila kitu kinatokea.Siku zile ukiingia kwenye Google,utaona maelfu ya watu wakilalamika jinsi ya kuyapangilia mafaili kwenye Windows Vista.Kwa mfano labda kuna picha ndani ya fali lako,basi mpangilio utaonesha jina,tarehe,tags,kama kuna tags nk.Yote haya yanafanya upate mambo papo kwa hapo.Pia kama unataka kutafuta kitu ndani ya windows 7,pindi uandikapo nacho kinaaanza kutafuta moja kwa moja kama inavyoonekana
  kwenye picha.

  [​IMG]
  2.XP Mode

  Hi ndio kitu ambacho kimenivutia mno kwenye Windows 7,kwani kuna baadhi ya programu ambazo labda mtu ulizinunua hapo awali ila haziwezi kutumia na operating sysytem nyingine.Kwa kutumia XP mode unaweza kufanikisha hili,pia kufanikisha hili ni rahisi mno,tembelea website ya Microsoft kwa ufafanuzi zaidi.Ila watakutaka wahakikishe kuwa umenunua nakala ya halali,hivyo kwa wenzangu na mimi wenge nakala bomu hapo lazima utakwama.  [​IMG]

  Kizuri hakikosi matatizo madogo,hapo awali ili kutumia XP mode ulitakiwa kutumia vitrualization,ila kuanzia mwezi wa tatu Microsoft wamesema XP mode haiitaji tena Virtualization,ni mwendo wa moja kwa moja tu.Hivyo kwa wale wenzangu na mimi ambao bado wanatumia Kompyuta za zamani hakuna hofu tena.

  3.Kushare mafaili

  Kwenye Windows 7 kubadilishana au kushare mafaili kumerahisishwa zaidi,ni kwa kwenda kwenye setting za Network na kubonyeza vitu vichache unakuwa tayari umeshaunganishwa kwenye intaneti au kushare mafaili na wenzako popote walipo.Hii kitu ilikuwa inasumbua sana kwenye XP ambapo ilihitaji mtu ambaye anafahamu Komputa kidogo kuweza kufanikisha hilo.

  [​IMG]  4.Muonekano

  Kusema kweli Windows 7 imejitahidi sana kwenye muonekano kulinganisha na matoleo mengine yaliyowahi kutoka hapo mwanzo,pia kwenye Windows 7 kama unataka kubadilisha muonekano,rangi,mpangilio ni kwa hatua chache mno tu unaweza kufanikisha hilo.Ni tofauti sana na matoleo yaliyopita ambayo inahitaji mtu mwenye mazoea kidogo ili kuweza kubadilisha kitu kidogo tu.  Hivyo basi haya ni machache ambayo mimi nimeyaona,je unafahamu lolote? Ungana nasi kwa kuchangia makala hii je ni kipi kinakuvutia kwenye Windows 7?
   
Loading...