Kwanini Watu Wenye (IQ Kubwa) Wanaongoza Kuwa na 'Mabushoke' Kwenye Ndoa na Mahusiano Kuliko Darasa la Saba?

Kwanini Watu Wenye (IQ Kubwa) Wanaongoza Kuwa na 'Mabushoke' Kwenye Ndoa na Mahusiano Kuliko Darasa la Saba?

Secret Star

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Posts
1,785
Reaction score
1,848
Kama wasomi na "Great Thinkers, sisi ni mabingwa wa kufanya Due Diligence ((upembuzi yakinifu). Ukitaka kununua kiwanja cha milioni tano Chanika, utaenda Wizara ya Ardhi, utaleta mpima ardhi wako, utahoji majirani, na utataka kuona hati halisi. Ukitaka kununua gari used la milioni 15, utaleta mafundi watatu tofauti wapime injini.

Lakini inapokuja kwenye kuingia ubia wa maisha (Ndoa/Mahusiano) na mtu ambaye atadhibiti 50% ya mali zako, asilimia 100 ya amani yako ya akili, na kuwa "Co-founder" wa watoto wakohapo ndipo wasomi tunapoweka akili pembeni na kutumia matope".

Hebu tuangalie makosa yetu ya kiuchambuzi kimkakati:

  • Mchakato Feki wa 'Interview': Kampuni ikitaka kuajiri mtu wa kumlipa laki nane, itapitia CV yake, itampigisha usaili wa mdomo na maandishi, na itampigia simu mwajiri wake wa zamani (Background Check). Lakini msomi akitafuta mwenza, "interview" yake ni kwenda mgahawani, kunywa juisi, kumuuliza "unapenda rangi gani?", na jamaa akijibu kwa sauti ya upole au mdada akiwa na tabasamu zuri—BOOM! Interview imepasiwa. Mwajiri wa zamani (MaEx) hawaulizwi kwanini mkataba ulivunjwa!
  • Kupuuza 'Rred Flags' (Auditing Failure): Wewe ni Mhasibu mzuri ofisini. Ukikuta hesabu hazibalansi, unakataa kusaini. Lakini kwenye mahusiano, unaona kabisa mtu ana Liability kubwa (hasira za karibu, mvivu, hajui kutafuta pesa, au anawasiliana na ma-ex wake saba). Badala ya kusitisha mkataba, msomi anasema, "Nitambadilisha kwa upendo wangu." Mkuu, huwezi kubadilisha Balance Sheet mbovu kwa kutumia upendo!
  • Hasara ya Mtaji (Initial Investment ROI): Wasomi tuko tayari kuchukua mkopo wa benki kufanya sherehe ya harusi ya Milioni 30 ili kuwafurahisha watu 400 ambao 350 kati yao hata hatuna namba zao za simu. Kwenye uchumi, hii ni sawa na kununua Depreciating Asset kwa mkopo wenye riba kubwa. Siku ya pili baada ya harusi, mnaanza maisha na deni, mkiangaliana usoni huku "Return on Investment" (ROI) ikiwa ni picha za kwenye albamu pekee.
  • Falsafa ya "At least ana hofu ya Mungu": Hii ndiyo Business Plan ya wengi. Tunatumia kigezo cha mtu kwenda ibadani kama kigezo cha yeye kuwa mwekezaji mzuri kwenye maisha. Tunasahau kuwa hata watu wanaofilisika kibiashara wana hofu ya Mungu. Kwenye ubia wa maisha, unahitaji mtu mwenye "Hofu ya Umaskini" na "Mikakati ya Kujenga Msingi," sio tu mtu wa ku-quote mistari ya vitabu vitakatifu huku bili ya umeme ikisomwa.
Hitimisho la Kikatil:Ndoa na mahusiano ndiyo Mkataba wa Kibiashara wenye hatari (Risk) kubwa kuliko yote duniani, lakini ndiyo mkataba ambao tunaingia kwa kutumia vigezo dhaifu kuliko vyote. Kama tungetumia hata 10% ya Critical Thinking tunayotumia kubishania siasa za uchaguzi kwenye kuchagua wenza, wengi wetu tungekuwa mbali sana kiuchumi na kiakili.

Nipo hapa kusikiliza mapovu yenu wakuu. Je, ni kweli upendo hauhitaji Risk Assessment? Uwanja ni wenu.
 
Watu wengi wenye IQ kubwa huwa wako low kwenye Emotional Quotient hivyo ni vyepesi sana kuwa zubaisha kwenye upande wa hisia,
Pia wengi hawana experience na mahusiano hivyo akitokea mtu akampatia vilivyo anahisi huyo ndo mwenyewe na atafanya chochote kwa ajili yake.
Tatu kwa kuwa wana akili sana hivyo anajihakiishia mwenyewei ni vigumu kudanganywa na hapo ndio watu wanamdanganya vizuri tu
 
Jomba unashindanisha Emotion over Logic. Mambo mawili tofauti.

Tafsiri kubwa ya mapenzi ipo upande wa hisia, Na wengi wanapoteana kwenye mapenzi kwasababu ya kubeba hisia mbele na kupumbaza mantiki.

Watu wenye ubwenke (akili)
kupitiliza, wapo vizuri kutafsiri mantiki lakini kwa swala la hisia wengi wanashindwa kutafsiri. hawajui kutafsiri mihemko ya kihisia inayo husiana na mapenzi, mapenzi yakiwakaba hawajui jinsi ya ku react kihisia, ndio sababu ya kuwa mabushoke.

Mapenzi hisia lakini ukitaka uzichape nyingi kama baltazar, lazima ubalance mzani wa logic na emotions. Leo unamwambia babe nikutoe out kesho unamwambia babe niko bize tutaonana vaada ya siku 3.
 
Comment Namba 5 hapo juu amejibi vizuri kabisa...
Hii ni battle ya Logic vs Emotions. Hapa logic haifui dafu linapokuja kwenye swala la mapenzi linaloamuliwa na hisia.......
 
Licha ya hizi mbanga na harakati..at the end watoto ndio waathirika wakubwa
 
Hakuna fundi wa Mapenzi!!....Kungwi mwenyewe ndoa 7 zimemshinda sijui anafunda nini!!!
 
Back
Top Bottom