Ni siku nyingine Tena, Tunamshukuru Mungu! Poleni Wafiwa wote.
Hivi Ulishawahi kujiuliza kwanini Watu /Mtu anaamua kuwa Muuwaji? Kwa Leo Hebu tuangalie sababu mbili au tatu hivi zitatosha. Kisha kwenye Mada zifuatazo tutajua kama kuna "remedy" ya kuwasaidia watu Kama hao.
Sababu mojawapo Huwa ni Visasi vya Muda mrefu, kuna baadhi ya watu wameumbwa kuweka visasi! Na watu Kama hawa huwa ni wagumu "kuachilia" mioyo yao na kusamehe! Mara nyingi watu Kama hawa huweza kuua Wahusika wote Kwa mpigo au mmoja mmoja au hata Kwa kuacha muda baada ya Muda. Kumbuka Mfano wa Yule jamaa wa Mkoani Mara ambaye alikua akiuwa watu kila alipopata chance. Ilikuja "kusemekana" kuwa chanzo ni visasi vya kudhulumiana.
Namba mbili haina tofauti Sana na namba moja Kama ilivyoishia. Watu au mtu hufikia Maamuzi ya kuua kutokana na dhuluma! Huyu nae anaweza kujikuta ameua watu wengi ili kufuta ushahidi! One scene, jamaa amemuua mtu lakini akagundua kuwa jirani mmoja ameona tukio. Hivyo aka-opt kumaliza mchezo lakini pia Wakati anamuua akagundua pia mtoto wake anashuhudia tukio hili. Hivyo anaamua kumuua pia.
Tatu, uhasama wa kimapenzi, manyanyaso, ubakaji, ukatili wa kingono na mambo Kama haya! Hawa huwa mara nyingi huja na "option" ya tukose wote au akose yeye! Hawa ni wengi Sana. Lakini pia hapa kuna wale ambao waliwahi kubakwa, au kuumizwa na Wapenzi wao, Mara nyingi suluhisho kwao ni moja tu, nitawamaliza!! Kuna cases nyingi Sana kwenye mitandao ambapo mtu anakwenda kumchukua "Dada poa" analala naye kisha anammaliza. Hufurahi kuona wamelipa kisasi.... Kwa Tz ndio wale watu unaosikia wakisema "Wanaume wote ni mbwa" au "Wanawake wote ni Malaya". Watu wa namna hii Huwa wamekua wamebeba maumivu makali Sana mioyoni mwao!
December 2018 Kijana mmoja alimuua msichana wake Wakati wakigombana.... Kisa simu! Well, ni sababu ndogo kwako lakini Kwa mwingine Inaumiza! Unaamua kuua!
2016 Bagamoyo, Kijana aliamua kumuua mchumba wake na Mtoto wake kwa kuwacharanga kwa mapanga kwa kinachosadikika kuwa ni Wivu wa mapenzi! Hapa, Tukisema tutaje basi kila mtu atakuja na Kisa chake, itoshe Kusema hivyo tu!!
Matumizi ya vilevi kupindukia huweza kusababisha Mauwaji pia, wapo watu ambao wakiisha kupata "addiction" ya kitu Fulani basi Huamini kuwa kuuwa ndio kupata kwao amani! Kwahio kila Wakati wanajisikia kuuwa tu, hata hapa jukwaani iliwahi kupostiwa Mada ya mwenzetu akitamani kuuwa! Ukianza kuuwa mmoja basi unajisikia raha na kutamani kuendelea....
Imani za kishirikina....wengine wamejikita huku kutokana na imani za kishirikina, huenda "the recent Njombe cases" zikawa Mfano mzuri hapa Kama zina ukweli. Ukiua mmoja Unatamani kuuwa mwingine....
Tutaendelea.....
Sent using
Jamii Forums mobile app