Kwanini watu wamezoea Kifo?

Status
Not open for further replies.

bonem

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
235
55
Habari wapendwa wanajukwaa,

Ninalo ombi kwenu. Siku hizi twaweza kwenye modern society, kifo kimeonekana kama ni kifo cha kawaida, hakipewi tena tafsiri ya kiimani au kimungu.

Mtu anapofariki tunakimbilia kusema amelogwa, kuna mkono wa mtu, amekufa ghafla, pengo lake halitazibika na majibu mengine ya kukatisha tamaa.

Kwanini watu wanataka kukizoea kifo? Au kwanini tunakataa kuona kifo kama kazi ya Mungu kuuchukua uhai ambao ni mali yake na kukimbilia kutafuta sababu nyingine za sisi wenyewe kutaka kuinesha kwamba tunaelewa sana kifo.

Karibuni mnisaidie tafadhali
 
Kwanza si kweli kwamba kifo kinazoeleka lakini pia tukichukulia kwa mtazamo wa Kimungu tuu ni makosa makubwa kwakuwa kuna imani nyinginezo zisizo amini uwepo wa Mungu
 
Kwanza kifo ni nini?
Kifo ni hali/kitendo cha mwili kupoteza utambuzi na kusimama kwa mifumo ya kibailojia na kikemia ambayo huufanya mwili kustawi na pia kujitambua.
*je lazima kifo kiwepo au kifo ni bahati mbaya/ajali?
Kwa miaka mingi falsafa na theolojia zimejaribu kuhoji juu ya kifo, baadhi ya hoja ni kuhusu kwanza chanzo cha uhai, kama zilivyo Nadharia nyingi na maandiko yanaeleza chanzo cha uhai, maandiko matakatifu (biblia na quran tukufu) vinaeleza kuwa chanzo cha uhai wa mwanadam na viumbe wengine ni Mungu, kwa hoja hiyo Mungu ndiye mwenye mamlaka juu ya uhai huo (kuzaliwa na kufa)

Kifo siyo bahati mbaya kwani ni kitendo bayana ambacho hutokea kwa mtu aliye hai au kiumbe yeyote mwenye uhai, kitu chochote chenye mwanzo wenye sababu zijulikanazo lazima hufikia mwisho wake ili kuthibitisha mwanzo wake, hivyo kifo kwa mtu ni ukamilifu j mwanzo wake, kila kifo kina sababu zake lakini lengo ni moja tu yaani "kufa". Kufa hakupaswi kuogopwa kwa maana ndiyo udhihirisho wa kuzaliwa/kuumbwa kwako.
*kwanini watu wamezoea kifo?
Kifo kama matukio mengine asilia kama kuzaliwa, huwafanya watu kuyatilia maanani kwa mda fulani tu, baadae huzoea maanaa binadam anauwepo wa kuzoea hali (coping with conditions) hivyo kuzoea ni uthibitisho tosha kuwa kifo kiko nje ya uwezo wa mwanadam, kama si hivyo wangefanya juhudi za kurudisha tena uhai wa mfu, lakini mwanadam hana uwezo huo (limited ability).
 
Kwa hiyo kama Mungu hahusiki na uhai wetu nani anahusika sasa? Vipi kuhusisha kifo na masuala ya ushirikina? Na kusema mtu amecha pengo kuna maana yoyote kweli
 
Hakuna binadamu anayezoea kifo au kuona Ni kitu cha kawaida,
Kila mtu huchukulia kifo kwa iman yake na ukaribu wa mfiwa mwenyewe na umri uliokuwa nao!
 
Kwa hiyo kama Mungu hahusiki na uhai wetu nani anahusika sasa? Vipi kuhusisha kifo na masuala ya ushirikina? Na kusema mtu amecha pengo kuna maana yoyote kweli
Labda nikuulize kwanza Una wazaz wote wawili ?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom