Kwanini watu wa Mbeya wanaendekeza ushirikina licha ya kuwa na madhehebu kila mtaa?

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Jela miaka minne kwa kufukua kaburi la albino Mbeya
|
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya imewahukumu watu wawili kila mmoja kifungo cha miaka minne jela na kulipa faini ya Sh2.3 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa kula njama na kufukua kaburi la marehemu aliyekuwa na ulemavu wa ngozi (albino). Washtakiwa hao wakazi wa Mbalizi walifukua kaburi la Sister Sisara (38) aliyefariki dunia mwaka 2008 na kuzikwa katika Kijiji cha Mumba, Kata ya Ilembo wilayani Mbeya.

Hakimu Rashid Chaungu aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Jonas John (28) na Hazore Ezekia (33). Akitoa hukumu, Chaungu alisema Mahakama imeridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilisha mashahidi watano.
508b2ed075495499804d6cd23669d8f1.jpg

Alisema katika kosa la kwanza kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili jela na kulipa faini ya Sh1 milioni. “Katika shtaka la pili, kila mmoja atalipa faini ya Sh1 milioni na kutumikia kifungo cha miaka miwili jela. Kwa sababu ya maelezo ya mashahidi wa upande wa mashtaka mlisababisha usumbufu kwa familia, mtailipa Sh300,000 kila mmoja,” alisema Chaungu.

[HASHTAG]#Mwananchi[/HASHTAG].

Na hili ni mbeya
Wavutaji Mbeya walalamika bangi kuadimika mtaani (Audio).

Hili nalo ni mbeya

Mbeya : mama afukua kaburi la mwanae
Hili nalo mbeya
Jamaa aliyekufa miaka 14 iliyopita afufuka na kusimulia maisha aliyokutana nayo alipokuwa

My take: Ushirikina kwa watu wa mbeya ni sawa na Teja na Ngada na uwepo makanisa kila mtaa ni kama kichaka cha kuficha maovu yao ya kishirikina kwa misingi hiyo asilimia kubwa ya waumini kutoka mbeya wanavinasaba vya kishirikina. Am sorry wana mbeya huo ndiyo ukweli. Kufufuka maiti ni nyinyi. Kupatikana kwa mtu aliyekufa miaka 14 iliyopita ni nyinyi. Kila kitu cha kichawi ni nyinyi.

TUKIO LINGINE LINALOHUSISHWA NA MAMBO YA KISHIRIKINA LATOKEA MBEYA:

Kikongwe wa miaka 100 aliwa na fisi.
|
Kikongwe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 100, Asyenepe Laia, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi.

Miaka 100 auawa na fisi

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya fisi hao kumuua, katika tukio lililotokea Alhamisi iliyopita, waliondoka na mwili wake kwenda katika msitu ulioko jirani na eneo analoishi na kula nyama yake.

Mashuhuda hao walisema katika tukio hilo, Asyenepe alikamatwa na fisi hao alipokuwa anaokota kuni ajili ya kuchochea katika moto alio kuwa ameuwasha ndani ya nyumba yake.

Walisema tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Kalulu Mashambani kandokando na Hifadhi ya Msitu Hifadhi ya Taifa ya Selous katika Tarafa ya Matemanga, Tunduru mkoani Ruvuma.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Dk. Gaufrid Mvile, alisema chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na kitendo cha wanyama hao kumshambulia.

Alisema katika tukio hilo walikuta mabaki ya vipande viwili vya mifupa, michirizi ya damu na mabaki ya nguo, mambo yaliyoashiria kuwa kikongwe huyo aliuawa na fisi hao na kumla nyama yake yote. [HASHTAG]#Nipashe[/HASHTAG]

MTAACHA LINI UCHAWI WATU WA MBEYA?
 
Ndo hapo unapotambua kuwa makanisa mengi yanayoibukia ni ya kishetani. Watu wengi wanajidai ni walokole lakini ndani ya mioyo yao ni mashetani wakubwa!
 
Jela miaka minne kwa kufukua kaburi la albino Mbeya
|
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya imewahukumu watu wawili kila mmoja kifungo cha miaka minne jela na kulipa faini ya Sh2.3 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa kula njama na kufukua kaburi la marehemu aliyekuwa na ulemavu wa ngozi (albino). Washtakiwa hao wakazi wa Mbalizi walifukua kaburi la Sister Sisara (38) aliyefariki dunia mwaka 2008 na kuzikwa katika Kijiji cha Mumba, Kata ya Ilembo wilayani Mbeya.

Hakimu Rashid Chaungu aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Jonas John (28) na Hazore Ezekia (33). Akitoa hukumu, Chaungu alisema Mahakama imeridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilisha mashahidi watano.
508b2ed075495499804d6cd23669d8f1.jpg

Alisema katika kosa la kwanza kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili jela na kulipa faini ya Sh1 milioni. “Katika shtaka la pili, kila mmoja atalipa faini ya Sh1 milioni na kutumikia kifungo cha miaka miwili jela. Kwa sababu ya maelezo ya mashahidi wa upande wa mashtaka mlisababisha usumbufu kwa familia, mtailipa Sh300,000 kila mmoja,” alisema Chaungu.

[HASHTAG]#Mwananchi[/HASHTAG]

My take: Ushirikina kwa watu wa mbeya ni sawa na Teja na Ngada na uwepo makanisa kila mtaa ni kama kichaka cha kuficha maovu yao ya kishirikina kwa misingi hiyo asilimia kubwa ya waumini kutoka mbeya wanavinasaba vya kishirikina. Am sorry wana mbeya huo ndiyo ukweli. Kufufuka maiti ni nyinyi. Kupatikana kwa mtu aliyekufa miaka 13 iliyopita ni nyinyi. Kila kitu cha kichawi ni nyinyi.

Mkuu Conflict of interest inanilazimisha katika uzi wako huu niwe ' mkodoaji ' sana kuliko ' mzozaji ' mno. Shikamoo!
 
Mkuu Conflict of interest inanilazimisha katika huu wako uzi niwe ' mkodoaji ' sana kuliko ' mzozaji ' mno. Shikamoo!
Haiwezekani kila aina ya mambo ya Giza yawe yanafanyika mbeya tu kwa kiasi kikubwa. Nimeku pm nikaona umefunga pm yako. Nilitaka nikuambie upite pale kwa mghaibuni japo humpendi ila siyo mbaya kuosha macho.
 
Wanachuna ngozi mbeya, wapiga nondo mbeya, wabaka vibibi mbeya, kwanini kila siku iwe mbeya isiwe pwani???? Hebu watu wa mbeya mjiangalie kwa nafsi ya pili.
 
Acha uzushi Weye pm yangu iko wazi 24/7 sema tu nimeiseti maalum kabisa iwe inachagua pm za Great Thinkers tu!
 
Wanachuna ngozi mbeya, wapiga nondo mbeya, wabaka vibibi mbeya, kwanini kila siku iwe mbeya isiwe pwani???? Hebu watu wa mbeya mjiangalie kwa nafsi ya pili.
Nadhani itakuwa vema sana wakija kutuambia nini hasa kinachoendelea hapo ?
 
Hawawezi kuja hapa mbeya wanasali masaa 12 wapo kanisani lakini kwa matukio wanaongoza jamani.
 
1.Upigaji wa NONDO
2.Utajiri wa Mbegu za Mahindi
3.Uchunaji NGozi etc huko ni balaaa
Kuna nini kinachosumbus hawa watu?. Madhehebu na dini nyingi zilizopo hapo mbeya ni kwa ajili ya kujifunzia mambo haya mabaya?
 
Tunaweza kuwa wavumilivu sana kama ilivyo asili yetu. Lakini tuhuma hizi zote zinatokea kwetu tu? Au umeamua kufanya mashambulizi kwa kuwa tu umekwazwa na mtu wa Mbeya? Unaweza kuwa na uhuru wa kuhoji but not th....
 
Wao ukiongea nao wanasema shetani hufanya kazi sana sehemu zenye upinzani mkubwa. Kwa maana kwamba wao ni washika dini sana, hivyo shetani anawafuatilia sana
 
Back
Top Bottom