Kwanini watanzania tusimiliki ardhi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini watanzania tusimiliki ardhi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nivea, Jun 25, 2012.

 1. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wanajamii naomba mnifungue kwenye hili jamani,hii ardhi yetu ni mali ya serikali mpaka lini?hivi na jirani zetu nao wako kama sisi kenya ,rwanda ,burundi , DUNIA NZIMA NA NCHI ZILIZOENDELEA etc,
  hili nimelizungumza kwa sababu hii kubwa ,mfano :umenunua kiwanja chako kwa bei kubwa sana bila msaada wowote wa serikali,kile kiwanja unakilipia kodi,then unajenga nyumba kwa gharama kubwa ambazo kila kifaa kuanzia tofali unalilipia kodi mpaka nyumba inaisha,ikimaliza wanapita tra kutathimini ,uaanza lipia tena ile nyumba kulingana na tathimini yao,swali linakuja hapa je hii nyumba inazalisha nini ilipiwe kodi,je ile kodi ninayolipia kwenye ujenzi siinakwenda serikalini?naona niunyonyaji wahaliyajuu sana,na kiasi kikubwa cha mapato kinarudi kulekule kilipotoka ! Ile ardhi sinilinunua mwenyewe? Na hii hela inatoka kwenye mshahara ambao tayari serikali imeshachukua kodi ,huwa naona ni unyanyasaji sana wawananchi .hii hela huwa inaniumiza sana!hata kuitoa huwa nashindwa tu kuilaani ipotee kabla haijafikishwa!
  Wana gt nifafanulieni kuhusu hili jambo naweza nisieleweke dhamira yangu ila kwa wanaojua swala hili watanifungua ,je kwanini ardhi hii isiwe mali yetu?kwanini tunalipa kodi kwa vitu ambavyo tumevigharamia kwajasho letu wenyewe bila msaada wa serikali na bila punguzo la bei ,na je nchi zote wanafanya hivi?
  Nahisi nimeeleweka ,nawakilisha wakuu?
  Ni kheri kuuliza kuliko kukaa nikilaumu nakuumia .
   
Loading...