Mimi ni mtanzania ambaye nina elimu ya kawaida (Degree) toka nje ya nchi, na kwa kiasi kikubwa nimetumia muda mwingi wa maisha yangu kufanya kazi nchi mbali mbali ulaya na amerika.
Nilichokiona katika nchi zetu za kiafrika ni kutukuzana kwa kuitana majina (titles) kulingana na elimu hasa baada ya mtu kutunukiwa degree ya PhD.
Ni jambo la kawaida kabisa kusikia mtu akimwita Dr. X ndani ya bar au hata katika mazingira ya nyumbani. Mtu na mke, au na mdogo wake wanahitana hivyo hivyo.
Hali hii ni ya ajabu zaidi inapotokea kwamba huyo mwenye elimu yenye title ya Dr. au Professor ni mwanasiasa na ni engineer. Kwa maana hiyo jina lake sasa linakuwa 'Mh. Dr. Eng. Msomi' (kwa mfano).
Niwe mkweli kwamba elimu yangu haijafikia level hiyo, lakini kwa uzoefu wangu wa zaidi ya miaka 25 nje ya Tzn sijawhi kusikia watu wa aina hiyo wakiitana majina kulingana na usomi wao.
Cha ajabu, hata hizo tuzo za degree za kupewa (honorary) nao wanajiingiza kwenye upuuzi huu.
Utasikia kwenye kanisa la mama Lwakatare anaibuka mtu anasema "Mh. Mchungaji Dr. Lwakatare".
Kwanini sisi waafrika tunatukuza kitu hiki na hasa wasomi wa leo hii? Mwl. J. K. Nyerere aliweza kutunukiwa degree za honorary nyingi tu, lakini sikuwa kusikia akiitwa Ndg. Dr. Mwl. Nyerere.
Kwa wale wanaojua Rais wa Marekani Baraka Obama msomi wa sheria katika katiba (Professor in Constitutional Law) lakini sijawahi kusikia huko marekani akiitwa President Prof. B. Obama.
Siku zote anaitwa President Obama, na wakati mwingine ni Mr. Baracka Obama. Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel ana PhD lakini kama walivyo wengine wengi katika nchi hizo sijawahi kusikia akiitwa Dr. A. Merkel ndani au nje ya bunge la Deutschland.
Sasa hapa kwetu mambo ndo hivo, Mh. Dr. Kikwete, Dr. Magufuli, Mh. Prof. Eng. S. Mhongo!! What's wrong mtu akaitwa tu Manji hapa kwetu Africa? Au wasomi wetu na wanasiasa wetu ni watu special?
Nawasilisha.