Kwanini wasomi hukimbilia nje ya nchi?

Kwanini wasomi hukimbilia nje ya nchi?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,456
Reaction score
69,361
Hivi ndugu zangu hili mnalionaje,nimebahatika kusoma na kukutana na watu wengi wenye uwezo mkubwa kitaaluma lakini mwisho wa siku wote hawataki kurudi nyumbani kufanya kazi.

Kuna dogo moja alisoma International School of Moshi akaenda Kusomea Mining Engineering University of Alberta na amefaulu vizuri kweli lakini hataki kurudi home.Ukiongea naye hataki kabisa kusikia anasema kuna siku alishawahi kuongelea mambo ya madini kwenye redio fulani akatishiwa na watu asiowajua.

Tena kuna jamaa yangu mwingine alisoma pale AGHA KHAN MZIZIMA akepelekwa kusoma AVIATION ENGINEERING MOSCOW STATE UNIVERSITY hataki rudi.

kuna wengine nawafahamu wamesoma Harvard,MIT,hadi Yale lakini hawataki hata kusikia kuhusu Tanzania yaani its sad. Kinachouma zaidi wengine wamemaliza UDSM,MUHIMBILI,MZUMBE miaka ya nyuma kidogo na wanajiweza haswaa ila wameshaondoka nchini.

Mimi nakumbuka mwalimu wangu moja hivi ni alisoma SOVIET UNION miaka ya nyuma na alivyorudi akawa anafanya kazi kama engineer wa ndege kipindi cha Nyerere. Kuna siku akajishauri aombe kazi British Airways wazungu walimpa ile kazi kwa haraka kweli.

Siku anafika Airport ya Uingereza anadakwa na polisi wa Uingereza kumbe Nyerere kapiga simu muda jamaa arudishwe Tanzania. Basi jamaa akarudi TZ.Cha kusikitisha kipindi cha Mkapa jamaa walimwondoa kazini wakasema hana Uwezo ila sasa Msiba wa Nyerere umetokea inabidi waende wakamkodi tena kutoka nje ili arekebishe ndege ya kumbebea Mwalimu.

Sasa mimi huwa najiuliza hivi ni kwanini wasomi wa Tanzania huwa hawakai nchini na hata kama akikaa nchini basi huwezi msikia anajihusisha na mambo ya maendeleo ya nchi.Mtu huyo awe Lawyer,.Engineer,Doctor,Economist,wooote hawataki kuisaidia nchi.

Yaani tunabaki na changamoto tupu.

 
wengi wanashawishika na "maslahi" remunerations nchi za abroad wanalipa vizuri kwa hizo kozi+securities, mfano ma doctor wengi hukimbilia botswana+canada+uk
 
Hivi ndugu zangu hili mnalionaje,
Nimebahatika kusoma na kukutana na watu wengi wenye uwezo mkubwa kitaaluma lakini mwisho wa siku wote hawataki kurudi nyumbani kufanya kazi.

Kuna dogo moja alisoma International School of Moshi akaenda Kusomea Mining Engineering University of Alberta na amefaulu vizuri kweli lakini hataki kurudi home...Ukiongea naye hataki kabisa kusikia anasema kuna siku alishawahi kuongelea mambo ya madini kwenye redio fulani akatishiwa na watu asiowajua.

Tena kuna jamaa yangu mwingine alisoma pale AGHA KHAN MZIZIMA akepelekwa kusoma AVIATION ENGINEERING MOSCOW STATE UNIVERSITY hataki rudi.

kuna wengine nawafahamu wamesoma Harvard,..MIT,...hadi Yale lakini hawataki hata kusikia kuhusu Tanzania yaani its sad.
Kinachouma zaidi wengine wamemaliza UDSM,..MUHIMBILI,...MZUMBE miaka ya nyuma kidogo na wanajiweza haswaa ila wameshaondoka nchini.

Mimi nakumbuka mwalimu wangu moja hivi ni alisoma SOVIET UNION miaka ya nyuma na alivyorudi akawa anafanya kazi kama engineer wa ndege kipindi cha Nyerere. Kuna siku akajishauri aombe kazi British Airways wazungu walimpa ile kazi kwa haraka kweli.

Siku anafika Airport ya Uingereza anadakwa na polisi wa Uingereza kumbe Nyerere kapiga simu muda jamaa arudishwe Tanzania. Basi jamaa akarudi TZ.
Cha kusikitisha kipindi cha Mkapa jamaa walimwondoa kazini wakasema hana Uwezo ila sasa Msiba wa Nyerere umetokea inabidi waende wakamkodi tena kutoka nje ili arekebishe ndege ya kumbebea Mwalimu.

Sasa mimi huwa najiuliza hivi ni kwanini wasomi wa Tanzania huwa hawakai Nchini na Hata kama akikaa nchini basi huwezi msikia anajihusisha na mambo ya maendeleo ya nchi...
Mtu huyo awe Lawyer,.Engineer,...Doctor,..Economist,...wooote hawataki kuisaidia nchi.

Yaani tunabaki na changamoto tupu.

Wewe CP kwanini usirudi kwanza?
 
wengi wanashawishika na "maslahi" remunerations nchi za abroad wanalipa vizuri kwa hizo kozi+securities, mfano ma doctor wengi hukimbilia botswana+canada+uk

Mbona zamani maslahi yalikuwa madogo sana lakini tulijisikia vizuri sana kurudi home.
Wazungu walitaka wengi tubaki huko lakini tulikataa kata kata. kuna kipindi tulivyorudi tulifanya hadi extra time bila hata malipo na we felt proud.

Sasa kwanini siku hizi wengi hawataki kubaki kusaidia nchi kama zamani?
Nini kinawafukuza?

 
Nenda hapo Rwanda kuna professor mmoja wakitanzania amezawaidiwa uraia wa Rwanda na PK! Muulize niaje aikimbia pale FoE? Jibu lake ni kwa swali ulilopost. Sawa?

Kwa bahati mbaya Professor Lwakabamba karudi kuendeleza kwao..
 
sababu nyingine ni kazi kutoka kwa kujuana, mtoto wa shangazi, mjomba, mtoto wa kigogo, hata kama una elimu yako, utakaa na vyeti mpaka kubadilika rangi, hii ndio tz,
 
kama wasomi wenyewe ni akina Dr slaa na prof liPUMBA wacha tubaki wapumbavu na malofa sisi ndio tuna uzalendo na nchi yetu
 
Muanzishaji wa mada hii amesema yule Engineer wa ndege alikodishwa kutengeneza ndege ya kumbeba Nyerere alipofariki.Naomba awe wazi zaidi.Ni ndege ipi hiyo....???ile Boeing iliyorushwa na Marehemu Cpt Lesani kutoka UK ikiwa na Mwili wa Nyerere au ile Fokka ya serikali iliyobeba mwili toka DAR hadi Musoma
 
Hivi ndugu zangu hili mnalionaje,nimebahatika kusoma na kukutana na watu wengi wenye uwezo mkubwa kitaaluma lakini mwisho wa siku wote hawataki kurudi nyumbani kufanya kazi.

  • Kuna dogo moja alisoma International School of Moshi akaenda Kusomea Mining Engineering University of Alberta na amefaulu vizuri kweli lakini hataki kurudi home.Ukiongea naye hataki kabisa kusikia anasema kuna siku alishawahi kuongelea mambo ya madini kwenye redio fulani akatishiwa na watu asiowajua.

  • Mimi nakumbuka mwalimu wangu moja hivi ni alisoma SOVIET UNION miaka ya nyuma na alivyorudi akawa anafanya kazi kama engineer wa ndege kipindi cha Nyerere. Kuna siku akajishauri aombe kazi British Airways wazungu walimpa ile kazi kwa haraka kweli. Cha kusikitisha kipindi cha Mkapa jamaa walimwondoa kazini wakasema hana Uwezo ila sasa Msiba wa Nyerere umetokea inabidi waende wakamkodi tena kutoka nje ili arekebishe ndege ya kumbebea Mwalimu.

Yaani tunabaki na changamoto tupu.



Mie naona unauliza swali na kutoa majibu mwenyewe, sasa sijui sie tukuwekee marks au? Si utapata 100%?
 
Muanzishaji wa mada hii amesema yule Engineer wa ndege alikodishwa kutengeneza ndege ya kumbeba Nyerere alipofariki.Naomba awe wazi zaidi.Ni ndege ipi hiyo....???ile Boeing iliyorushwa na Marehemu Cpt Lesani kutoka UK ikiwa na Mwili wa Nyerere au ile Fokka ya serikali iliyobeba mwili toka DAR hadi Musoma

Good,
inaonyesha ulikuwepo.
Ukweli unaujua.
 
BongoNyosooooo.................. Nitakuja October 25 (kuichinja CCM) ofcoz niko na kitambulisho kipya cha mpiga kura
 
Niliona kwenye ITV boeing ikituwa tena on time kabisa na nikamuona cpt.Pia niliona kwenye ITV ile Fokka ya serikali ikiruka kwenda Musoma.niliuliza hivyo kwa kujuwa engineers wa ndege walikuwepo ATC na pia kwenye kitengo cha ndege za serikali na wanauwezo wa kurekebisha matatizo endapo yatatokea na hakukuwa na haja ya kumleta engineer toka nje.Bado nina ukakasi na hiyo mada.Nina waamini sana marubani wa kitanzani na mafundi wetu wa ndege waliopo nchini.
 
Nina waamini sana marubani wa kitanzania na mafundi wetu wa ndege waliopo nchini.

They are pretty good!!!
but ni kwanini wanakimbia chini yao?
 
Back
Top Bottom