Kwanini Wanaume ndio wanaongoza kwa kujinyonga? Case Study ya Marekani

Kwanini Wanaume ndio wanaongoza kwa kujinyonga? Case Study ya Marekani

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
79,254
Reaction score
85,128
Sababu za Wanaume Kujinyonga sana ni zipi hasa?

---
79% ya waliojiua Marekani 2022 ni Wanaume

Marekani imeweka rekodi ya kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu waliojiua mwaka jana, ambapo zaidi ya watu 49,000 walijiua mnamo 2022, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na serikali.

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), vilichapisha data mpya siku ya Alhamisi ambapo takwimu zilionyesha kuwa wanaume walikuwa ni asilimia 79, ya jumla ya idadi ya watu waliojiua mnamo 2022.

Wataalamu wanaonya kwamba ongezeko hili linaweza kusababishwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na viwango vya juu vya mfadhaiko na upatikanaji mdogo wa huduma za afya ya akili.

Makamu Mkuu wa Rais wa Utafiti katika Wakfu wa Marekani wa Kuzuia Kujiua Jill Harkavy-Friedman ameongeza kuwa kichocheo kikuu ni kuongezeka kwa upatikanaji wa bunduki nchini humo.

Uchambuzi wa hivi majuzi wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, ulitumia data ya awali ya 2022 kukokotoa kwamba kiwango cha jumla cha watu waliojiua kwa kutumia bunduki kilipanda mwaka jana hadi kiwango cha juu zaidi na kwa mara ya kwanza, kiwango cha kujiua kwa bunduki miongoni mwa vijana Weusi kilipita kiwango cha vijana weupe, watafiti waligundua.

Hadi sasa watu wengi bado wanaamini kuwa kuomba msaada ni ishara ya udhaifu.
 
Waafrika tuna raha sana. Hao wanaoishi huko majuu - Wamarekani na wazungu wote hawana maisha kabisa. Elewa maisha sio mali na utajiri peke yake.

Maisha ni pamoja na uhuru wa kufurahi na kuchangamana na wengine bila kujali umevaa nini, umekula nini, una nini. Ukienda kwenye mikusanyiko angalia kama kuna wazungu... utaona wanavyoenjoy maisha yetu ya kula, kunywa na kucheza pamoja; hasa vilabuni... watu wanafurahi hata kama sio ndugu na hawajuani.

kujinyonga ni ugonjwa wa akili. Akili inafikia ukomo wa kufikiri na inaona suruhisho ni kujinyonga. Jichanganye , be happy no matter what.

Lisilowezekana haliwezekani tu. Usilazimishe wala kuumiza moyo wako kwa kitu ambacho umeshindwa kuwa nacho.

Leo furaha deiiiii karibuni kamyweso, tukaimbe na kucheza pamoja 🤣
 
Well ni shida kubwa, lakini isitokee tukawatweza wanaofika tamati yao kwa mtindo huo sababu hatujui huwa wanapitia hali gani hadi kufikia hatua hiyo.

Dunia imejaa matatizo mengi yanayotegemea akili ya mwanaume kutatuliwa na uwezo wa kila mtu kuhimili hali upo tofauti.

Yule akikosa kazi anakuwa normal mimi nikikosa kazi akili inaruka so mimi nadhani ni mwisho alioandikiwa mtu wa kuumwa ataumwa afe wakujiua atapewa shida kama sababu ili ajiue.
 
Back
Top Bottom