Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau, amani iwe kwenu.
Tangu zoezi la utumbuaji majipu lilipoanza, tumeshuhudia watu kadhaa wakijitokeza na kupinga zoezi hilo. Mtu wa kwanza kulalamika ni aliyekuwa mgombea Urais wa CHADEMA na UKAWA kwenye uchaguzi wa Oktoba 2015, Edward Lowasa ambaye kwa upande wake alisema kuwa Rais Magufuli anawatumbua watu kwa itikadi za kisiasa kwa hisia kuwa waliunga mkono upinzani. Pia alisema kuwa Rais anatumbua watu ambao hakuwateua yeye na ndo maana hana huruma nao.
Mtu wa pili kupinga utumbuaji huo ni Freeman Aikael Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa jimbo la Hai. Mbowe alitokwa na povu jingi kwa kusema kuwa utumbuaji huo haufuati katiba na sheria hasa haki ya kusikilizwa.
Baada ya makamanda hao wawili kuongea, tukaanza kusikia kelele nyingi kutoka kwa vibaraka wao wakiwemo wanaojifanya watetezi wa haki za binadamu. Pia kelele hizo tumeanza kuziona humu mitandaoni. Binafsi nimejiuliza sana. Hii huruma ya CHADEMA kwa wanaotumbuliwa imeanza lini? Nini maslahi yao kwa wanaotumbuliwa majipu? Je utumbuaji huu wa majipu unahatarisha nini kwa ustawi wa CHADEMA na UKAWA?
Swali kubwa zaidi ambalo limenifanya nije mbio kuomba ushauri kwa wadau ni hili. kama utumbuaji majipu unafanyika bila kufuata Katiba, Sheria na Kanuni, KWA NINI MPAKA SASA WANAOLALAMIKA NA KUPINGA UTUMBUAJI MAJIPU SI MIONGONI MWA WANAOTUMBULIWA? kuna nini hapa? Mpaka sasa hakuna hata mmoja aliyejitokeza hadharani kupinga kutumbuliwa kwake. Kama katiba na sheria zinakiukwa kama anavyosema Mbowe, iweje sasa hao wanaotumbuliwa hawataki kwenda Mahakamani kudai haki yao? Kuna nini hapa?