mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Hakika inashangaza sana kuona waendesha Bodaboda wanafunja sheria mbele ya askari wa usalama barabarani bila kukamatwa na kuchukulia hatua za kisheria hali ambayo inawafanya waendelee kuvunja Sheria.
Bodaboda hao wamekuwa wanabeba abiria zaidi ya mmoja (mishkaki) na kupita mbele ya askari wa usalama, Bodaboda wamekuwa wanaendesha bila kuvaa kofia, lakini askari wapo na wanaona.
Bodaboda wamekua wanapita kwenye mataa licha ya taa kuwazuia hali ambayo in hatari kiusalama lakini askari wa zamu anayeongoza magari anaona na hachukui hatua zozote.Bodaboda hao wamekuwa wanatumia kwa makusudi barabara za mabasi ya mwendo kasi licha ya sheria kuwakataza hali ambayo inaweza kusababisha ajali.
Tunaliomba Jeshi letu la Polisi lijitahidi kwa nguvu zote kuwadhibiti Bodaboda hawa kwani wamekuwa wanasababisha ajali Mara Kwa Mara.Pia tunaliomba Jeshi la Polisi litoe adhabu Kali ili waogope.