Kwanini Waafrika wanateswa na kufukuzwa Israel?

Hakuna mweusi anaefukuzwa Israel ,inamaana wasipofata taratibu za uhamiaji waachwe mkuu?mim ninekuwa Israel for the last two months hawana shida so long unafata sheria ,waangalie wamarekani walivyowapenda wayahudi na ndio taifa lilifanikiwa na uchumi mkubwa dunian
 
Wahabeshi wangapi wamefia kwenye magari wakipita na wale wanaopona wanawekwa magerezani? Wakimbizi wa kirundi au Rwanda walishapewa kazi kama siyo kuwekwa makambini na misaada siyo ya tanzania bali ya UN. Hawa wakienda Israel wanaishi kuwa mitaani na kuwa omba omba.
Wewe umefika Israel kuona wakimbizi wanaoenda kule wanavyotunzwa? wana matunzo mazuri kulinganisha na hawa tunaowasweka lupango na wengine kuishia makambini. Naongea kwa kuwa shahidi kutokana na kazi yangu.
Ila lazima udungwe sindano ya kuzuia usizae mkuu, Taifa lenu teule Hilo
 
Ila lazima udungwe sindano ya kuzuia usizae mkuu, Taifa lenu teule Hilo
Kama unasoma habari sasa hivi angalia mtu aliyeua watu 20 texas manifesto yake. He mentioned unti semitic with other races. Sasa Myahudi bila kujilinda na amezungukwa na maadui ulimwengu mzima afanyeje? Wayahudi wenye asili ya Ethiopia mbona walichukuliwa wakati wa njaa na mpaka sasa wame integrate kwenye society.
 
Mayahudi ni shida
 
Hao ni wale waliokarilishwa kitabu kitakatifu.....ambao wanaamini juu ya taifa teule....Zamani nilikua sielewi kwanini Mwl JK Nyerere alikua hawafagilii hawa jamaa wakati Mwalim ni Mkristo na hata ubalozi wao umefunguliwa juzi tu na JPM...Nilipokua na kuacha kushikiwa akili na kutafakari mambo kwa kina nikajua Mwl alikua sahihi.
Hawa jamaa kwanza nchi wanayoclaim kuwa ni yao waliyopewa na Mungu, kwenye bible inasemekana kuwa ni ya maziwa na asali cha ajabu mi naona jangwa tu pale...as a reasonable man siwezi kuamini kama hili ni taifa teule wakati kuna vingi walivyojibebesha kwenye bible haviko hivyo....ila ukiwaambia wenzangu na mimi wanakuona umepotoka.

Binafsi point yako nimeipenda!

Ni kweli kabisa ukizungumzia Israel, watu wengi hukimbilia kwenye dini bila kujua kuwa wao (Israel) wanapotetea maslahi yao huwa hawahangaiki na kinachoitwa "dini" bali maslahi yao kama nchi huwa yanatangulizwa mbele na hiyo siyo kwa wao tu bali kila Taifa lenye viongozi wanaojielewa wanatakiwa kutanguliza maslahi ya wananchi wao mbele.

Kingine Wakristo wengi huchukulia ile dhana ya Yesu Kristo kuzaliwa nchini Israel kwa kudhani kwamba watu wote wa enzi hizo walikuwa wafuasi wake, si kweli kulikuwa na Serikali ya kirumi chini ya Pontio Pilato na magavana kama Herode na wengineo, hivyo Yesu alionekana kama tunavyowaona akina Gwajima, Mzee wa Upako, Oyedepo na wengine wa aina hiyo, na ndiyo maana nchini Israel Wakristo wenye asili ya kiyahudi ni wachache (Wana dini yao na kitabu chao)

Yesu amekuwa maarufu baada ya kuondoka duniani na hiyo ni baada ya watawala waliokuwa na nguvu enzi hizo (Roman Empire) kulishwa mafundisho yake na mtume Paulo kisha nao kuyasambaza kwenye makoloni yao. hii ilichagiza kuja na msemo wa kiswahili unaosema "Nabii hakubaliki kwao" (hisia zangu)

Binafsi nionavyo mimi ni kuwa utakatifu wa Israel au uharamu wake na mengine kinyume na hayo havitusaidii chochote kuelekea kwenye uchumi wa kati bali tunatakiwa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu ili bara letu na nchi yetu Tanzania isonge mbele kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.
 
Hakuna mweusi anaefukuzwa Israel ,inamaana wasipofata taratibu za uhamiaji waachwe mkuu?mim ninekuwa Israel for the last two months hawana shida so long unafata sheria ,waangalie wamarekani walivyowapenda wayahudi na ndio taifa lilifanikiwa na uchumi mkubwa dunian

Kwa hiyo mkuu inawezekana China napo kuna Wayahudi, maana nasikia inamnyanyasa Marekani kiuchumi!!?
 
at certain time in the future hii democracy itabidi tuidefine upya!..
Hivi whats special with Uganda, nakumbuka Israel kabla hawajawekwa walipo sasa ilikuwa wapewe eneo Uganda kuanzisha taifa lao.
2ngeteseka sana asee east africa
 
Back
Top Bottom