Kwanini Viongozi wa Simba SC wanatudanganya mashabiki?

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Ujue tunawavumilia sana lakini amtaki kutuonea huruma hata kidogo,kwanza tuna uchungu sana kukosa ubingwa msimu huu na bado munatudanganya

1. Maamuzi ya kamati ya hadhi na Sheria yalipotoka kwanini amkuenda FIFA hadi ligi imeisha

2. Mumetuma nakala kwa DHL hata wiki haijapita halafu munatuambia Jumanne yani kesho wanatolea maamuzi. Hivi iyo kamati ilikuwa inawasubiri nyingi

3. Hivi FIFA wanaweza kutoa maamuzi kwa kuwasikiliza nyie tu bila kumsikiliza Mwanachama wake TFF. Dah umeona wapi maamuzi ya upande mmoja

4. Mzigo wenu mulio upeleka FIFA mbona hamjatuambia kama umefika?
5:Report ya mchezo ni confidential document ya Tff je Simba sc mutaitoa wapi,nani atakaye wapa,na kama mumeipeleka Fifa mumeipataje bila kutoa Rushwa

Mnatuletea Siasa mjue tumewachoka musitufanye mambumbu sasa. Haya tuone kesho si ndio munapewa ubingwa na FIFA sasa tusipoupata mtuachie ofisi zetu.
 
Moja kati ya washabiki wanaojielewa, Viongoz wa Simba wanatumia propaganda ya kuonewa na TFF kuwazingua kwani walivyokua mbele kwa tofauti ya point 8 nini kiliwasibu? Kwa nini msingewafunga tu Kagera ili kutokua na huu utata? Jibu simple waliwazid uwezo
 
Wewe yanga kaogelee swimming pool imejaa
Hapo ndo umeonyesha umbumbumbu kabisaaaa.. Huyu jamaa awe Yanga au awe Simba, alichoongea kikufungue akili ya Mgando ulonayo! Alichoongea jamaa ni kweli kbs.... Unachopaswa kujua ni kwamba, hauna viongozi, una wauza maneno... Jamaa ni wanasiasa kabisa,.. Wamewajengea akilini kuhusu point tatu.... Hivi zile point nane mngekomaa nazo mngekaa kusubiri ushindi wa kuzawadiwa wa mezani? Mlipoteza mechi, kwanini wanashindwa kuwajibika? Ninyi mnaweza kuongozwa hata na GIGY MONEY
 
Dawa yao ni kesho Na tuta andamana yale maandamano waliyotaka tuyafanye kwa ajiri ya KUDAI point tatu tutaandana kuwa toa madarakani.Ligi imeshaisha , Ubingwa kesho pewa Yanga Basi time ilikuwa mbele Kwa point nane Leo mnakuja kutuambia point za mezani ndio maana Kocha anasema alaumiwe yeye kunakitu hapo. Tu naomba mtuache msimuamshe aliye lala
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu ataelewa kuwa:
1. Kagera Sugar na Simba zote zilichezesha wachezaji 11
2. Simba ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar
3. Kamati ya saa 72 kilikuwa 'kikao cha send-off'
4. Kipa wa Mbao FC alihongwa na Simba
5. Toto Africa waligoma kupokea mpunga wa Simba Koko
6. Mbao ni kiboko ya Yanga
7. Manara ni 'mhuni'
8. TFF ni chama cha mpira wa miguu na sio Table Tennis au Pool Table
9. Yanga hawakosi ubingwa eti kwa kutishiwa OKWI na Korie
10. Dar Young Africans ni bingwa mara 27 bila MEZA

Navyofahamu mimi, mpira ukichezwa Kaitaba matokeo hayawezi kutokea Zurich.
 
Simba mna tabu kweli, kubalini matokeo yaishe..Hizo point za mezani achaneni nazo
 
Back
Top Bottom